Fahari ya Serengeti

Sunday, January 11, 2015

VICOBA MOROTONGA WANUFAIKA NA MFUKO WA JIMBO LA SERENGETI

 Wanachama wa vikundi vinne vya Vicoba kata ya Morotonga wilaya ya Serengeti wakiwa wamekaa wakisubiri utaratibu wa kupokea sh 1 milioni kutoka mfuko wa jimbo,ambapo kwa kila kikundi wamepata sh 250,000
 wakiwa pamoja katika eneo la ofisi ya CCM ambayo pia hutumiwa na mtendaji wa kata hiyo.
 kabla ya kupewa kiasi hicho cha fedha walitakiwa kusaini kupokea
 Utaratibu unaendelea.
 Vikundi hivyo vina jumla ya wanachama 120

 Mwenyekiti wa kitongoji cha Morotonga Bruno akifungua kikao
 Afisa mtendaji wa kata hiyo Paulo Wangwe akitoa ufafanuzi wa fedha hizo na angalizo kwa wanufaika

 Katibu wa mbunge wa jimbo la Serengeti Gabriel Mwita akiwasainisha viongozi wa vikundi vilivyopata msaada huo kabla ya kuwapa fedha hizo
 Mwenyekiti wa kikundi cha Mkulima Theresia Charles akisaini kupokea kiasi cha sh 250,000 kwa niaba ya wanachama 30
 Wanasaini


 Anashukuru kwa niaba ya wenzake
 Wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya pamoja

Friday, January 9, 2015

MAFUNZO YA KUPINGA UKEKETAJI KWA WATOTO 134 WALIOKIMBILIA NYUMBA SALAMA KANISA LA ANGLIKANA MUGUMU SERENGETI YAHITIMISHWA

 BAADHI YA WATOTO WALIOKIMBIA KUKEKETWA WAKIWA WANAONYESHA IGIZO JUU YA MADHARA YA UKEKETAJI WAKATI WA KUHIMISHA MAFUNZO KWENYE NYUMBA SALAMA ILIYOKO KANISA ANGLIKANA WILAYA YA SERENGETI DAYOSISI YA MARA,AMBAPO JUMLA YA WATOTO 134 KUTOKA MAENEO MBALIMBALI WALIKIMBIA KUKEKETWA.
 IGIZO LINAENDELEA
 UJUMBE UNATOLEWA KWA JAMII KUHUSU MADHARA YA UKEKETAJI

 WANAWASILISHA UJUMBE ILI JAMII IACHANE NA MFUMO HUO UNAOSABABISHA MADHARA KIAFYA
 BAADHI YAO WAKIFUATILIA IGIZO
 WANAFUATILIA
 WADAU MBALIMBALI WANAOPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA WALIKUWEPO,IKIWEMO NA DAWATI LA JINSIA LA POLISI SERENGETI
 WANASEMA NYUMBA SALAMA NI KIMBILIO LA WANAPINGA VITENDO VYA UKATILI WA KIJINSIA.
 UJUMBE UJUMBE,UJUMBE KILA KONA



 ASKOFU ELIKIA OMINDO WA KANISA LA ANGLIKANA DAYOSISI YA MARA AKITOA UJUMBE

PICHA YA PAMOJA



Thursday, January 8, 2015

SAKATA LA KUTELEKEZWA MAITI POLISI

 MSAFARA WA WATU MBALIMBALI WAKIELEKEA KITUO CHA POLISI MUGUMU WILAYA YA SERENGETI WAKIPELEKA MAITI YA MZEE SAMSONI NYAKIHA(70)MKAZI WA BONCHUGU ALIYEFIA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO  CHANZO KIKIDAIWA NI KIPIGO KUTOKA KWA ASKARI WA HIFADHI YA SENAPA NA POLISI WAKIMTUHUMU KUJIHUSISHA NA UJANGILI WA TEMBO,
 SAFARI INAENDELEA
 WANAELEKEA POLISI
 BAADHI YA NDUGU NA WATU WENGINE WALIOFUATILIA MKASA HUO WAKIWA NJE YA UZIO WA KITUO CHA POLISI WAKISUBIRI MUAFAKA JUU YA SAKATA HILO.

 WANAFUATILIA
 JENEZA LINAPELEKWA NDANI YA KITUO CHA POLISI ,KWA MADAI KUWA TOKANOVEMBA 16 MWAKA JANA ALIPOPIGWA NA KUPOTEZA FAHAMU ALIKUWA CHINI YA ULINZI WA POLISI,HIVYO WALIWARUDISHIA POLISI MTUHUMIWA WAO.
 JENEZA LINAINGIZWA POLISI
 OCD NA WASAIDIZI WAKE WAKIWA WAMESHIKWA NA BUMBUAZI WAKIJADILIANA NINI KIFANYIKA.
 NDUGU NAO WAKIWA WANAJADILIANA HUKU WAKISISITIZA MSIMAMO NI MMOJA MPAKA WAAMBIWE ALIYEHUSIKA NA KUMPIGA NA HATUA GANI ZIMECHUKULIWA
 BAADA YA MAJADILIANO MAREFU POLISI WANAKUBALI MWILI WA MAREHEMU UKAHIFADHIWE HOSSPITALI TEULE YA NYERERE WAKATI WAKITAFUTA MUAFAKA,GARI LA POLISI LILIHUSIKA KUBEBA.

 TARATIBU ZINAENDELEA


 WATU WANASUBIRI HATIMA YAKE

 HAPO WANAJIANDAA KWENDA HOSPITALI

 NDUGU WA MAREHEMU WAKIWA KITUO CHA POLISI



 WANAELEKEA HOSPITALI

 BAADHI YA WANANCHI WANAFUATILIA