Wilaya ya
Serengeti Mkoa wa Mara imefungua kitabu
cha michango ili kusaidia wakazi wa Mkoa wa Kagera walioathirika na tetemeko
la ardhi lililosababisha vifo vya watu 17 ,zaidi ya 200 kujeruhiwa na nyumba na
mali kuharibiwa.
Mkuu wa
wilaya hiyo Nurdin Babu akiongea na Serengeti Media Centre Afrika Ofisini mwake amesema
pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali kupitia kwa Waziri Mkuu,nao
wameamua kuweka utaratibu wa kuchangia michango mbalimbali kutoka kwa watu
watakaoguswa ikiwa ni fedha na vitu ili viweze kuwasaidia wananchi
walioathirika.
Amesema kila
mwananchi anatakiwa kuguswa na tatizo hilo kwa kuwa limeacha madhara makubwa
kwa wananchi wa mkoa huo,njia hiyo ndiyo inayoonyesha uzalendo wa kweli.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment