MSIHAMASISHE
KILIMO BILA KUWATAFUTIA MASOMO WAKULIMA.
Serengeti
Media Centre.
.Watendaji
wa serikali mkoa wa Mara wameombwa kuacha tabia za kuhamasisha wananchi kulima
mazao bila kuwatafutia masoko.
Mkuu wa Mkoa
wa Mara Dk Charles Mlindwa akiwa ziarani wilaya ya Serengeti alisema viongozi
wanatakiwa kuwa wabunifu wa kuwatafutia masoko wakulima ili kusaidia kuinua
uchumi wao.
Alisema ili
kuondokana na dhana hiyo ambayo imechangia wakulima kukata tamaa ,kwa kutambua
udhaifu wa watendaji wengi ofisi yake inaandaa program maalum ya uzalishaji
ambayo utasaidia upatikanaji wa masoko ya mazao mbalimbali yanayozalishwa
mkoani humo.
“Mkoa
unazungukwa na wawekezaji wa sekta mbalimbali ambao wanakosa huduma bora za
mali zinazozalishwa hapa na kufuata
maeneo mengine hadi nje ya nchi,ni wajibu wa watendaji wa halmashauri kuwa na
program maalum nini wanahitaji na kuwasaidia wakulima kuzalisha kwa ubora
unaotakiwa,hiyo ndiyo njia ya kuonyesha tija kwa kila mtendaji,”alisema.
Alisema
watendaji wengi wanakaa sehemu muda mrefu lakini tija yao haionekani,”watoto
wanaposhindwa mwalimu hulaumiwa kwa kuwa ufanisi wake huonekana mdogo,sasa kuna
tija gani kwa mtaalam kupokea fedha
wakati hatatui matatizo ya wananchi,huwezi kuhimiza wananchi walime wakati huna
suluhisho la soko harafu
ukajivuna,lazima uje na mipango,”alisema.
Kwa upande
wa mifugo alisema mkoa huo umekuwa lango la kupitisha na kupeleka nchi jilani
,”mifugo ni zao lazima wataalam wasaidia
wafugaji kufanya mabadiliko kwa kuacha kuhesabu utajiri wao kwa wingi wa mifugo
bali watumie uzito na ubora wa mfugo kwa kuwa thamani yake itakuwa juu,”alisema
na kuongeza,
“Miongoni
mwa mapinduzi makubwa tunatarajia kufanya ni kujenga kiwanda cha nyama mkoani
hapa ,hii itatusaidia kuongeza ubora wa mifugo na pia watu watafuga mifugo
michache iliyoboreshwa na hapo itakuwa imesaidia kupunguza migogoro ya maeneo
ya malisho na sekta nyingine,”alisema.
Diwani wa
Kata ya Nyansurura Francis Garatwa alisema ongezeko la mifugo katika maeneo
yaliyoko pembezoni mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni tishio kubwa kwa jamii
na kuwa kuwepo mpango mahsusi ambao utanusuru migogoro ya kuvamia hifadhi.
Mwisho.
0 comments:
Post a Comment