Wanafunzi wa shule ya Msingi Mapinduzi wilayani Serengeti na wadau wengine wamejitokeza
kupinga vitendo vya ukeketaji kwa maandamano na jumbe mbalimbali.
Viomgozi mbalimbali wa ngazi ya wilaya,asasi za ndani na nje ya nchi wameshiriki katika kufikisha ujumbe siku ya kupinga ukeketaji duniani.
Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Cosmas Qamara akitoa msimamo wa serikali,ambapo amesema wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka jana asilimia 72 ya wasichana waliokuwa wameandaliwa kukeketwa hawakukeketwa kutokana na kampeini kali zilizotanguliwa na elimu kupitia Mradi wa Tokomeza ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa tanzania kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)asasi mbalimbali za kijamii,Polisi,na viongozi wa dini kwa Ufadhili wa UN WOMEN,ngariba tisa walikamatwa kati yao wawili wameishahukumiwa na wazazi wawili.
Wadau wakiwa katika Picha ya Pamoja katika Kituo cha Nyumba Salama mjini Mugumu,
Wakiwa katika Picha ya Pamoja
Wanaandamana wakiwa na jumbe mbalimbali,
Maandamano kupita mjini yakiendelea
Elimu ndiyo msingi wa mtoto wa kike si kumkeketa.
Wanapaza sauti wanaendelea kuvunja ukimya.
Wanapaza sauti.
Askari wa Usalama barabarani wakiongoza.
Wazazi wanafikiria kukeketa watoto wanapewa somo.
Usalama wao umezingatiwa.
Burudani zilikuwepo
Wanafikisha ujumbe kwa njia za nyimbo.
Ujumbe kutoka kwa viongozi mbalimbali,kamanda wa upelelezi makosa ya jinai wilaya ya Serengeti Alfredy Kyebe akielezea jinsi Polisi wanavyopambana na masuala ya ukeketaji.
Afisa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji wilaya ya Serengeti William Mtwazi akielezea mikakati mbalimbali ya kutokemeza ukeketaji wilayani humo.
Wanafuatilia nasaha mbalimbali
Mratibu wa Nyumba Salama Rhobi Samweli akielezea madhira yanayowakuta watoto wanaokimbia kukeketwa na jinsi wanavyowasaidia kituoani hapo.
0 comments:
Post a Comment