Fahari ya Serengeti

Friday, February 3, 2017

WADAU WA MAHAKAMA WATAKIWA KUTUMIA MUDA VIZURI ILI KUHARAKISHA KESI

 Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti Ismael Ngaile akielezea mikakati ya Mahakama kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati katika siku ya Sheria nchini.


 Baadhi ya wazee wa Mahakama ya Mwanzo wakifuatilia burudani na nasaha kutoka kwa viongozi mbalimbali walioshiriki maadhimisho hayo.
 Burudani ya asili maarufu kama ritungu ina raha zake kama inavyoonekana hapo,mwanamama licha ya kuangusha kanga hakujali bali ni muziki kwa kwenda mbele.
 Wasanii wa ngoma ya asili Ritungu wakiburudisha watu waliohudhuria maadhimisho hayo.
 Picha zilipigwa kama inavyoonekana.
 Mambo yanaenda yakiongezeka ,muziki uliwakuna wengi na kujitosa uwanjani,ngoma ya asili ina vionjo vyake.
 Mgeni Rasmi Paulo Shanyangi kushoto kwa niaba ya Dc Nurdin Babu akiingia eneo la tukio ,kulia ni Hakimu Mkazi mafawidhi wa wilaya Ismael Ngaile.
 Kila mmoja akienda kuchukua nafasi yake.
 Heshima iliyolewa.

 Mkurugenzi wa Ukaguzi na Usimamizi wa  Maadili Mahakama ya Tanzania Warsha Sylvester Ng'humbu akitoa nasaha kwa mahakimu,waendesha mashitaka,mashahidi na wapelelezi kuhakikisha wanatumia muda vizuri kumaliza kesi kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua uchumi na kupunguza gharama kubwa za kuendesha kesi.
 Mkuu wa Magereza wilaya akisalimia
 Maombi yalitolewa kama anavyoonekana hapo Mchungaji wa Kanisa la Anglican Mugumu
 Mchungaji Cleophace Nyamataga wa kanisa la Kmt akimwaga maombi kama inavyoonekana.


 Watoto waliokimbia uketaili wa kinjisia (kukeketwa)kutoka maeneo mbalimbali na ambao wanahifadhiwa Kituo cha Nyumba Salama waliimba nyimbo za kuiomba Mahakama kutoa adhabu kali kwa watu wanaoendekeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

 Watu mbalimbali walikuwepo.
 Paul Shanyangi kwa niaba ya Dc akitoa hotuba
 Watu kutoka mataifa mbalimbali walifuatilia matukio ya siku hiyo muhimu ambayo ni kuanza kazi kwa majaji Tanzania,mwaka wa kimahakama unaanza.
 Kila mmoja ana njia yake ya kuchukua kumbukumbu za siku hiyo kama inavyoonekana.
 Wapo waliotunukiwa vyeti kwa maana ya kutambua mchango wao wa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
 Hakimu Ngaile alikuwa miongoni mwao baada ya mchango wake kutambuliwa na wadau mbalimbali nje ya mahakama.
 Anapata cheti.






Hata wazungu walishiriki kuimba na kucheza.

0 comments:

Post a Comment