Magari mawili yametolewa na Frankfurt Zoloogical Society imetoa magari mawili kwa Senapa na Ikona kwa ajili ya kuboresha utendaji na kuimarisha doria ili kupunguza migogoro kati ya wananchi na wanyama katika maeneo ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo wilayani Serengeti.
Mkurugenzi wa Frankfurt Tanzania Gerald Bigurube kulia akiwa ameshikilia funguo za gari la Ikona Wma lenye thamani ya sh 79 mil lililotolewa na Umoja wa Ulaya (EU)kupitia shirika la FZS ili kuiwezesha jumuiya hiyo inayoundwa na vijiji vitano kuimarisha ulinzi katika ikolojia ya serengeti.
Afisa maliasili wilaya ya Serengeti John Lendoyan kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa gari hilo kabla ya kukabidhi viongozi wa Jumuiya hiyo,
Mkurugenzi wa FZS kulia akikabidhi Funguo kwa mhifadhi ujilani Mwema wa Senapa Nuhu Daniel Kwaniaba ya Mhifadhi Mkuu wa Senapa William Mwakilema,gari hilo limetolewa na Benki ya Maendeleo ya watu wa Ujerman KFW kwa thamani ya zaidi ya sh 70 mil,jumla ya thamani ya magari yote ni sh 150 mil.
Wanaangalia stika
Maandalizi ya kukabidhi.
Kikao kabla ya makabidhiana kinaendelea
Masegeri Tumbuyo meneja ujilani Mwema FZS akieleza lengo la kununua magari hayo.
wadau mbalimbali wameshiriki.
Afisa maliasili wilaya akieleza umuhimu wa uhifadhi kwa jamii.
Wanafuatilia
Askari wa Ikona nao walikuwepo
Anawasha gari mara baada ya kukabidhiwa
Ana jaribu gari
Kazi imeanza kama inavyoonekana.
Mijadala mbalimbali ilikuwepo
Wanyama hawakuwa mbali na eneo la tukio la makabidhiano.
Wednesday, May 31, 2017
Home »
» FRANKFURT YATOA MAGARI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH 150 MIL KWA SENAPA NA IKONA
0 comments:
Post a Comment