Fahari ya Serengeti

Friday, May 26, 2017

MCHIMBAJI DHAHABU MMOJA AFA WAWILI WANUSURIKA

 Ndugu na jamaa wa Mwita Gugwe Mkazi wa kijiji cha Mrito wilayani Tarime wakilia baada ya kufika katika mgodi wa kienyeji wa wachimbaji wadogo kijiji cha Merenga wilayani Serengeti alikofia kufuatia kuangukiwa na kifusi wakati wanachimba dhahabu,watu wawili wamenusurika katika tukio hilo.

Aprili mwanzoni mwaka huu katika shimo hilo watu wawili walikufa na mmoja kunusurika baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wanachimba dhahabu,hata hivyo uchimbaji huo ulisitishwa na Mkuu wa wilaya Nurdin Babu kwa masharti kuwa watakaoruhusiwa wanatakiwa kuwa na leseni ya uchimbaji.
 Mkuu wa wilaya Nurdin Babu Kulia akitoa maelekezo ya kufunga shughuli za uchimbaji na kuwataka watu wote watoke katika eneo hilo hadi watakapokata leseni na kuwaagiza askari polisi kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.
 Wanaangalia machimbo yaliyosababisha kifo
 Wamefia humu ndani
 Ndugu wakilia kwa uchungu baada ya kufika eneo la tukio.
 Wachimbaji wakimsikiliza Dc mara baada ya kufika enei la tukio.
 Dc akiwa akitoa msimamo wa serikali kuhusiana na tukio hilo,ameagiza kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji hadi taratibu za kisheria zitakapokamilika
 Ndugu wakiwa kwenye majonzi
 Baada ya kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji wanachukua viroba vyao ili kupisha eneo hilo.


0 comments:

Post a Comment