Fahari ya Serengeti

Tuesday, May 16, 2017

WAZEE WA MILA KOO SITA ZINAZOJIHUSISHA NA UKEKETAJI WAKUTANA

 Wazee wa mila wa koo za Inchugu,Inchage,Watatoga,Waryenchoka,Wangoreme na Wakenye wilayani Serengeti wamekutana kujadili Unyago Pasipo ukeketaji chini ya Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa tanzania,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na wadau mbalimbali.
Lengo ni kuhakikisha jamii inabadilika na kufanya unyago bila ukeketaji ili kuwaepusha watoto wa kike na ukatili unafanyika wakati wa ukeketaji.
 Wazee wakiwa wanafuatilia maelezo kutoka kwa watalaam wa amref juu ya unyago bila ukeketaji.
 Mjadala unaendelea

 Meneja Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti(amref)Godfrey Matumu akieleza umuhimu wa kufanya unyago bila ukeketaji,utaratibu ambao umefanikiwa Samburu nchini Kenya na Kilindi Tanga.


 Sungura Mtani mwenyekiti wa mila ya Inchage kwa Kenya na Tanzania akichangia hoja ya unyago bila kukeketa.
 Mijadala ya wazee wa koo mbalimbali wakiwa nje ili kujenga uelewa wa pamoja kabla ya kutoa maelezo
 Wanaelekea Ukumbi wa kanisa Katoliki Mugumu kwa ajili ya kuanza kikao.

0 comments:

Post a Comment