Fahari ya Serengeti

Thursday, May 18, 2017

WAZEE WA MILA KOO SITA WASAINI MAKUBALIANO YA KUACHA UKEKETAJI SERENGETI

Baadhi ya wazee wa mila wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin babu na viongozi wengine baada ya kikao maalum ambacho kimeshirikisha Koo za Inchage,Inchugu,Watatoga,Wangoreme,Wakenye na Warenchoka na  wamesaini makubaliano ya kuacha ukeketaji na badala yake watafanya unyago bila kukeketa,chini ya Mpango wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na wadau wengine kwa ufadhili wa UN WOMEN
 Wazee wa mila wakisaini makubaliano ya kuacha kukeketa watoto wilayani Serengeti.
 Wazee wa koo ya Inchugu na Inchage wakitoa tamko rasmi la kuacha ukeketaji.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiongea na wazee wa mila wa koo sita zinazojihusisha na ukeketaji,ambapo ameagiza ngariba na wazee watafute mashamba walime badala ya kutegemea fedha za ukeketaji kwa kuwa serikali haitawaacha salama.
 Anasisitiza jambo
 Naweka saini kuwa sitajihusisha na ukeketaji,mzee wa mila anaonekana akiweka makubaliano.



 Picha ya Pamoja ilipigwa
 Hao wameshiriki kuweka makubaliano hayo



mazungumzo yaliendelea kati ya mkuu wa wilaya na mzee wa mila wa koo ya Wakenye

0 comments:

Post a Comment