Kamanda wa Polisi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Mathew Mgema akiwa ameshikilia kombe baada ya timu ya Polisi Fc kuibuka bingwa wa kombe la Mei mosi kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Seronga Fc.
Pamoja na kombe wamepata sh 100,000 na mpira mmoja.
Timu ya mpira wa mikono wanawake ya Polisi nayo imeibuka bingwa baada ya kuifunga timu ya Chuo cha Uganga na uuguzi ya Kisare kwa mabao 12-2 na kupata kitita cha sh 50,000.
Wanashangilia ushindi
Tumeshindaaburudani hizo zimepamba maadhimisho ya mei mosi wilaya ya Serengeti
Wachezaji wa timu ya mikono wanawake ya Polisi wakiwa wamepozi na kikombe chao kufuatia ushindi wa mabao 12-2 dhidi ya Kisare,Hongereni sana.
Wanapongezana
Mpambano wa mpira wa mikono wanawake,Kisare walikubali kupigishwa kwata na polisi kwa mabao 12-2.
Kwaya ya walimu imekonga nyoyo wageni na wananchi ambao wamehudhuria maaadhimisho ya mei mosi na mkuu wa mkoa kuahidi kuitumia hiyo wakati wa ziara ya Rais mkoani humo.
Skauti nao walikuwepo
Wageni wameshindwa kujizuia na kuamua kwenda kuserebuka.
Monday, May 1, 2017
Home »
» POLIS FC NA POLISI QUEENS MABINGWA WA MAKOMBE YA MEI MOSI
0 comments:
Post a Comment