Fahari ya Serengeti

Sunday, November 27, 2016

AFIA NDANI YA SHIMO LA DHAHABU



AFIA NDANI YA SHIMO LA DHAHABU,

Serengeti Media Centre.

Mchimbaji mmoja wa dhahabu katika kijiji cha Nyamokobiti kata ya Majimoto wilayani Serengeti Mkoa wa Mara amekutwa ndani ya shimo la dhahabu akiwa amekufa huku akiwa na jeraha kichwani.
Tukio hilo ambalo limeibua maswali mengi linadaiwa kutokea usiku wa kuamkia novemba 26 mwaka huu katika shimo linalomilikiwa na John Ugolo lililoko katika eneo la Bigeso Mantago mkazi wa kijijini hapo,limethibitishwa na Polisi na uongozi wa kijiji na kata ambao wamemtaja aliyekufa kuwa ni Maro Matiko(45)ambaye ni ndugu na mmiliki wa shimo hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Ramadhani Ng’anzi akiongea na Serengeti Media Centre amemtaja aliyekufa kuwa ni Maro Matiko(45)na kudai kuwa hakuna mtu wanayemshikilia kwa kuwa hiyo taarifa wanaichukulia kuwa ya kawaida.

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Kebegi Nyamori ameiambia Serengeti Media Centre  kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio amesema,maiti iligunduliwa novemba 26 majira ya saa 2 asubuhi baada ya kukuta tochi aliyokuwa anaitumia kwa ulinzi nje ya shimo nay eye akawa haonekani.
“Siku ya tukio walikuwa wamepanga kwenda kijijini kwao Ring’wani na ndugu yake ambaye ni mmiliki wa shimo baada ya kuuza dhahabu ,Ugolo alilala kijijini na Matiko(marehemu)alilala nje ya shimo kama mlinzi ili watu wasiingie kuchimba,akawa amelewa viroba,inaonekana aliteleza akiwa amesinzia na kutumbukia na kupiga kichwa kwenye miamba,”alisema.
Alisema baadhi ya wachimbaji walishuka shimoni wakidhani anaendelea na kazi ya uchimbaji na kumkuta amekufa,”hata hivyohawakusubiri polisi wala uongozi wa kijiji walimtoa nje ndipo wakatoa taarifa kwangu nami nikajulisha polisi kwa ajili ya uchunguzi wa tukio zima maana hakuna mwenye maelezo sahihi jinsi ilivyotokea”alidai.
Kwa upande wake mwenye eneo hilo Bigeso Mantago alisema alipata taarifa za tukio kupitia kwa John Ugolo,hata hivyo alisema nje ya shimo alipokuwa amelala kama mlinzi walikuta  tochi na pakti za viroba hali ambayo inadhihirisha kuwa alikuwa amelewa.
Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walisema tukiohilo limetokea ikiwa ni siku chache baada ya ndugu hao kupata dhahabu ambayo waliuza na kupanga kwenda kijijini kwao Ring’wani huku wakiwa wamesitisha shughuli mpaka warudi,hata hivyo hakuna aliyekuwa na uhakika wa kiasi walichopata.
“Hili ni tukio la kwanza kutokea kwenye eneo langu limetushangaza sana ,lakini katika maeneo ya uchimbaji hapa ni la pili kufuatia tukio la kwanza kwenye shimo la Mndore Marungu mchimbaji mmoja alikufa baada ya kuzidiwa na moshi wakati wakitoa maji kwa jenereta,”alisema mmoja wa wakazi wa kijiji hicho.
Mwisho.


Friday, November 25, 2016

UONGOZI WA KIJIJI CHA MOSONGO SERENGETI WAAHIDI KUWAKAMATA WATAKAOKEKETA WATOTO WA KIKE

Wakazi wa kijiji cha Mosongo kata Mosongo wilayani Serengeti wakifuatilia mada za athari za ukeketaji kutoka kwa wataalam wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa tanzania na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC).

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji hicho Itembe Makorere amesema hatakubali kukamatwa yeye kwa kuwalinda wanaokeketa watoto kinyume cha sheria ,bali watakuwa wa kwanza kutangulia polisi.

Amesema elimu iliyokwisha tolewa na makatazo ya vyombo vya dola kuwa ukeketaji ni kosa la jinai yeye kama kiongozi wa serikali hatawafumbia macho wale wote wanaoendesha vitendo vya ukeketaj






Wanafuatilia mada

Baadhi ya wazee wa mila wa kijiji cha Mosongo wakifuatilia mada,hata hivyo kundi hilo linalotajwa kuwa kinara wa ukeketaji kwa kutangaza tarehe,kuandaa ngariba na mamvo ya kiufundi lilitoa msimamo wake kuwa hawatahusuka na ukeketaji wa watoto wa kike bali watashughulika na tohara za watoto wa kiume.
Kamanda wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wilaya ya Serengeti Alfredy Kyebe akifafanua vifungu vinavyokataza ukeketaji na adhabu yake ambayo ni kifungo kisichopungua miaka mitano na isiyozidi miaka kumi na tano.
Meneja wa Mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti (amref)Godfrey Matumu akisisitiza jamii kujikita kuwasomesha watoto wa kike badala ya kuwakeketa kwa kuwa watoto wengi wanakataa kufanyiwa ukatili huo na baadhi wanakimbilia katika kituo cha nyumba salama .
Mtumishi wa Mungu Genya akifafanua vifungu vya biblia vinavyoharamisha ukeketaji .

Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mosongo Itembe Makorere amesema watakaompelekea kadi za sherehe za kukeketa watoto wa kike badala ya kuwapa zawadi atawakamata na kuwafikisha polisi kwa kuwa ni kosa la jinai kwa mjibu wa sheria .

Wanapika huku wakifuatilia mada
Balozi wa amref Christopher Genya akielezea umuhimu wa kusomesha mtoto wa kike kwa wakazi wa Mosongo.
Wanafuatilia.
Monica Nyeura kutoka kitengo cha Mama na Mtoto wilaya akitoa mada ya athari za ukeketaji kitabibu kwa niaba ya Mganga mkuu wa wilaya Salum Manyatta.

Wanafuatilia mada kwa makini
Joseph Mrimi mwenyekiti wa Ritongo akielezea umuhimu wa kusomesha watoto wa kike

Wanafuatilia.





Wednesday, November 23, 2016

WATU WAWILI WADAIWA KUUAWA NDANI YA HIFADHI YA SERENGETI

 BBaadhi ya wakazi wa kijiji cha Mbirikiri kata ya Sedeko wilayani Serengeti wakilia kwa uchungu kufuatia taarifa za watu wawili wakazi wa kijiji hicho kudaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi na askari wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakati wanawinda ,na mmoja kujeruhiwa ,hata hivyo juhudi za kupata miili ya watu wanaodhaniwa kuuawa hazijazaa matunda baada ya kukuta mizoga ya nyati na viatu vya mmoja wa watu hao katika eneo la tukio,uchunguzi wa tuki unaendelea.

 Mbunge wa jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akiwapa pole wakazi wa kijiji Mbirikiri kuhusiana na taarifa ya maafa ya watu wawili na mmoja kujeruhiwa ambaye pia anashikiliwa na jeshi la polisi.



Friday, November 18, 2016

WAZEE WA MILA KOO YA NGOREME WAPIGA MARUFUKU UKEKETAJI

 Baadhi ya wazee wa mila ya koo ya Ngoreme na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye mkutano wa jamii maarufu(Ritongo)katika kijiji cha Mesaga kata ya Kenyamonta wilayani Serengeti ,mbali na kujadili mambo mbalimbali walitoa tamko la kupiga marufuku ukeketaji wa watoto wa kike kwa jamii hiyo,na kuwa watakaokaidi serikali ichukue hatua kali .
 Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Ritongo kijiji cha Mesaga
 Wanafuatilia






 Afisa mradi wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na Amref na Lhrc kwa ufadhili wa UN WOMEN ,William Mtwazi akifafanua hitaji la sheria kwa wanaojihusisha na ukeketaji.


Kamanda wa Upelelezi Makosa ya Jinai wilaya ya Serengeti Alfred Kyebe akielezea umuhimu wa jamii kutii sheria bila shuruti

KANISA LA AGAPE WUEMA SANCTUARY MINISTRIES KUJENGA HOSPITALI YA RUFAA NA CHUO MUSATI SERENGETI

Diwani wa kata ya kibanchabanche Philemon Chacha(wa pili kushoto)akimuonyesha Askofu mkuu wa Kanisa la Agape Martin Gwila(kushoto) eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Rufaa.
Viongozi wakuu kutoka kanisa la Agape Wuema Sactuary Ministries International wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu(wa pili kushoto mstari wa mbele)mara baada ya mazungumzo yalifanyika katika ofisi ya mkuu wa wilaya.
Mwenyekiti wa kijiji cha Musati Daudi Mgendi(aliyenyoosha mkono)akitoa maelekezo kwa viongozi wa kanisa la Agape mara baada ya kuwasili katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa Hospital.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Agape Martin Gwila(wa pili kushoto)akiteta jambo na baadhi ya viongozi mara baada ya kuwasili katika eneo la ujenzi wa Hospital ya Rufaa katika kijiji cha Musati.


Waendesha pikipiki almaarufu kama bodaboda wakiongoza msafara wa Viongozi kwenda kuangalia eneo la ujenzi wa Hospitali katika kijiji cha Musati.


Viongozi wa Dini na viongozi wa Serilaki wakiwasili katika shule ya msingi Musati kwa ajili ya kuongea na wananchi wa kijiji hicho mara baada ya kupokea eneo walilopewa kwa ajili ya ujenzi.
Baadhi ya Viongozi na wananchi wakikagua mradi wa Maji katika kijiji cha Musati.
Askofu Martin Gwila Akipongezana na mkewe Agness Martin mara baada ya kupokea eneo lenye takribani ekari 500 kwa ajili ya ujenzi wa Hospital ya Rufaa.
Diwani wa Kata ya Kebanchabanche Phillemon Chacha akisalimiana na wananchi wake katika mkutano uliofanyika shule ya msingi Musati.
Maaskofu wa Kanisa la Agape Wuema Ministry wakifanya mazungumzo na Katibu Tawala wilaya ya Serengeti Donald(wa nne kushoto) Kamara mara baada ya kuwasili ofisini kwake.
Diwani kata ya Kebanchabanche Philemon Chacha akitoa utambulisho kwa wananchi kuhusiana na ugeni uliowasili kijijini hapo.
Mwenyekiti wa kijiji cha Musati Daudi Mgendi akiwashukuru wananchi wake wakioudhuria kikao cha makabidhiano ya kiwanja kwa viongozi wa kanisa la Agape Wuema Ministry.


Askofu Mkuu wa Agape Wuema Ministry Martin Gwila akitoa Shukurani kwa wananchi wa kijiji cha Musati mara baada ya kupokea eneo kwa aijili ya ujenzi wa Hospital ya Rufaa.
Wananchi wa kijiji cha Musati wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wakuu wa Dini kutoka kanisa la Agape Wuema katika mkutano uliofanyika shule ya msingi Musati.
Askofu Godmon kutoka mkoani Morogoro akifanya maombezi kabla ya kuanza kwa mkutano na wananchi wa kijiji cha Musati kata ya Kebanchabanche.
Askofu Martin Gwila akifurahi mara baada ya kukabidhiwa Zawadi ya Mbuzi kutoka kwa wazee wa Mila kijiji cha Musati kata ya Kebanchebanche.
Mzee wa Mila Kisamarwa(wa pili kushoto) akimkabidhi Askofu Martin Gwila zawadi ya Mbuzi kwa niaba ya wazee wa mila wa kijiji cha Musati.