Isaya Petro Mkazi wa Mtaa wa Chamoto kata ya Stendi Kuu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amehukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kosa la kuharibu mali,ametakiwa kutengeneza nyumba alizoharibu na asipatikane na kosa lolote.
Aprili 6 mwaka huu Isaya aliezua mabati nyumba mbili za familia akimshinikiza mke wake ahame ili auze mji kwa kile kinachodaiwa kuwa hana faida kwa kuwa anamzalia watoto wa kike tu.
Kutokana na ukatili huo mke na watoto wake wanaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga kinacholipwa na wananchi wa mtaa huo.
0 comments:
Post a Comment