Ded Serengeti Juma Hamsini akiunga mkono Kauli mbiu ya Jenga Hospitali kwa sh 1000 kwa kutoa sh 1000,000 muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka kumaliza kukagua ujenzi wa hospitali hiyo na kuwasilisha ahadi yake ya Tsh 1 mil aliyotoa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa januari mwaka huu .
Hata hivyo amewasilisha michango mingine toka kwa wadau wa maendeleo aliokutana yenye jumla ya thamani ya tsh 7 mil .
Amesisitiza wananchi hasa wakazi wa wilaya hiyo kuunga mkono Kauli mbiu hiyo kwa lengo la kupata fedha za kukamilisha baadhi ya majengo ya hospitali ambayo inategemewa kutoa huduma kwa wakazi wa mkoa huo ikiwemo watalii.
Mambo yanazidi kuongezeka Patricia Kabaka akimuunga mama yake kutekeleza Kauli mbiu ya Jenga hospitali kwa sh 1000 kwa kuchangia sh 150,000.
Mwenyekiti wa CCM wilaya Jakobo Bega akiwasilisha risti ya mifuko 30 ya saruji yenye thamani ya Tsh 600,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya.
Mwenyekiti wa Uwt wilaya naye hakubaki nyuma
Diwani viti maalum Helana Sambayeti akichangia ujenzi wa hospitali
Tuesday, April 17, 2018
Home »
» JENGA HOSPITALI KWA SH 1000 YAZIDI KUCHANJA MBUGA
0 comments:
Post a Comment