Fahari ya Serengeti

Thursday, April 26, 2018

KANISA KATOLIKI KUITANGAZA HIFADHI YA SERENGETI

 Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma Michael Msonganzila amesema kanisa hilo limeanzisha mpango mahsusi wa kutangaza hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuwa ni uumbaji wa Mungu alioufanya kwa makusudi ambao unatakiwa kuenziwa na kila mtu.
Akizindua nyumba ya Tafakuri itakayotumika kama kituo cha mapadri na waumini Parokia ndogo ya Serengeti ambayo itatumika kupumzika na kujifunza mambo mbalimbali,pia wanaandaa eneo maalum ambalo litatumiwa na makundi mbalimbali yanayokwenda na kutoka  hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupumzika eneo hilo.
 Askofu Msonganzila akifafanua jambo kwa waumini waliohudhuria ufunguzi wa nyumba hiyo.
 Askofu akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri waliohudhuria misa ya ufunguzi wa nyumba hiyo.
 Maandamano kutoka Nyumba ya Tafakuri kwenda kanisani kwa ajili ya kuanza misa takatifu

 Baraka zinatolewa
 Utepe ukakatwa
Waumini wakifuatilia matukio mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment