Fahari ya Serengeti

Thursday, April 26, 2018

KWAYA YA MT.MARIA YAKONGA NYOYO ZA WAUMINI

 Kwaya ya Mt.Maria Mama wa Mungu Parokia ya Mugumu Jimbo Katoliki Musoma imekonga nyoyo za waumini kwa kuimba nyimbo zenye ujumbe mzito wakati wa Misa ya Ufunguzi wa Nyumba ya Tafakuri Parokia ndogo ya Serengeti iliyoongozwa na Baba Askofu Michael Msonganzila.
Askofu ameshindwa kuficha furaha yake na kuwamwagia sifa hasa mpiga kinanda mwanamke aliyeonyesha umahiri wake na kudai katika jimbo zima mtaalam huyo wa kike anapatikana kwaya hiyo na Parokia ya Mugumu tu.


 Wanakwaya wakiwa wanafuatilia matukio mbalimbali wakati wa misa takatifu
 Wakiongoza maandamano ya kuingia kanisani kwa ajili ya kuanza misa,
 Wanakwaya wakiendelea kuimba nje ya kanisa kabla ya kufungua nyumba ya Tafakuri
 Misa inaendelea
Wanaendelea kuhubiri kwa njia ya nyimbo.

0 comments:

Post a Comment