Fahari ya Serengeti

Wednesday, May 31, 2017

FRANKFURT YATOA MAGARI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH 150 MIL KWA SENAPA NA IKONA

 Magari mawili yametolewa na Frankfurt Zoloogical Society imetoa magari mawili kwa Senapa na Ikona kwa ajili ya kuboresha utendaji na kuimarisha doria ili kupunguza migogoro kati ya wananchi na wanyama katika maeneo ya vijiji vinavyounda jumuiya hiyo wilayani Serengeti.
 Mkurugenzi wa Frankfurt Tanzania Gerald Bigurube kulia akiwa  ameshikilia funguo za gari la Ikona Wma lenye thamani ya sh 79 mil lililotolewa na Umoja wa Ulaya (EU)kupitia shirika la FZS ili kuiwezesha jumuiya hiyo inayoundwa na vijiji vitano kuimarisha ulinzi katika ikolojia ya serengeti.
 Afisa maliasili wilaya ya Serengeti John Lendoyan kwa niaba ya Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa gari hilo kabla ya kukabidhi viongozi wa Jumuiya hiyo,

 Mkurugenzi wa FZS kulia akikabidhi Funguo kwa mhifadhi ujilani Mwema wa Senapa Nuhu Daniel Kwaniaba ya Mhifadhi Mkuu wa Senapa William Mwakilema,gari hilo limetolewa na Benki ya Maendeleo ya watu wa Ujerman KFW kwa thamani ya zaidi ya sh 70 mil,jumla ya thamani ya magari yote ni sh 150 mil.
 Wanaangalia stika
 Maandalizi ya  kukabidhi.
 Kikao kabla ya makabidhiana kinaendelea
 Masegeri Tumbuyo meneja ujilani Mwema FZS akieleza lengo la kununua magari hayo.
 wadau mbalimbali wameshiriki.
 Afisa maliasili wilaya akieleza umuhimu wa uhifadhi kwa jamii.
 Wanafuatilia
 Askari wa Ikona nao walikuwepo
 Anawasha gari mara baada ya kukabidhiwa
 Ana jaribu gari
 Kazi imeanza kama inavyoonekana.
 Mijadala mbalimbali ilikuwepo


Wanyama hawakuwa mbali na eneo la tukio la makabidhiano.

Friday, May 26, 2017

MCHIMBAJI DHAHABU MMOJA AFA WAWILI WANUSURIKA

 Ndugu na jamaa wa Mwita Gugwe Mkazi wa kijiji cha Mrito wilayani Tarime wakilia baada ya kufika katika mgodi wa kienyeji wa wachimbaji wadogo kijiji cha Merenga wilayani Serengeti alikofia kufuatia kuangukiwa na kifusi wakati wanachimba dhahabu,watu wawili wamenusurika katika tukio hilo.

Aprili mwanzoni mwaka huu katika shimo hilo watu wawili walikufa na mmoja kunusurika baada ya kuangukiwa na kifusi wakati wanachimba dhahabu,hata hivyo uchimbaji huo ulisitishwa na Mkuu wa wilaya Nurdin Babu kwa masharti kuwa watakaoruhusiwa wanatakiwa kuwa na leseni ya uchimbaji.
 Mkuu wa wilaya Nurdin Babu Kulia akitoa maelekezo ya kufunga shughuli za uchimbaji na kuwataka watu wote watoke katika eneo hilo hadi watakapokata leseni na kuwaagiza askari polisi kuimarisha ulinzi katika eneo hilo.
 Wanaangalia machimbo yaliyosababisha kifo
 Wamefia humu ndani
 Ndugu wakilia kwa uchungu baada ya kufika eneo la tukio.
 Wachimbaji wakimsikiliza Dc mara baada ya kufika enei la tukio.
 Dc akiwa akitoa msimamo wa serikali kuhusiana na tukio hilo,ameagiza kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji hadi taratibu za kisheria zitakapokamilika
 Ndugu wakiwa kwenye majonzi
 Baada ya kusitishwa kwa shughuli za uchimbaji wanachukua viroba vyao ili kupisha eneo hilo.


Thursday, May 18, 2017

WAJITOKEZA KUPIMA AFYA NA KUTOA DAMU


 Wakazi wa Mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti wamejitokeza kwa wingi kupima afya zao na kutoa damu kwa hiari chini ya uratibu wa Jopo la Wauguzi wilayani hapa,
 Wananchi wanatakiwa kujitokeza kuchangia damu kwa hiari kwa kuwa hospitali Teule ya Nyerere na maeneo mengine inakabiliwa na upungufu wa damu.


 Wataalam wakiwa kazini katika eneo la Uwanja wa Mbuzi mjini Mugumu.
 Uchangiaji wa damu unaendelea


Anachangia damu kwa ajili ya kuokoa akina mama wajawazito,watoto na wahitaji wengine wakiwemo wa ajali.

WAZEE WA MILA KOO SITA WASAINI MAKUBALIANO YA KUACHA UKEKETAJI SERENGETI

Baadhi ya wazee wa mila wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin babu na viongozi wengine baada ya kikao maalum ambacho kimeshirikisha Koo za Inchage,Inchugu,Watatoga,Wangoreme,Wakenye na Warenchoka na  wamesaini makubaliano ya kuacha ukeketaji na badala yake watafanya unyago bila kukeketa,chini ya Mpango wa Tokomeza Ukeketaji Serengeti unaotekelezwa na amref health africa,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu(LHRC)Halmashauri na wadau wengine kwa ufadhili wa UN WOMEN
 Wazee wa mila wakisaini makubaliano ya kuacha kukeketa watoto wilayani Serengeti.
 Wazee wa koo ya Inchugu na Inchage wakitoa tamko rasmi la kuacha ukeketaji.
 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiongea na wazee wa mila wa koo sita zinazojihusisha na ukeketaji,ambapo ameagiza ngariba na wazee watafute mashamba walime badala ya kutegemea fedha za ukeketaji kwa kuwa serikali haitawaacha salama.
 Anasisitiza jambo
 Naweka saini kuwa sitajihusisha na ukeketaji,mzee wa mila anaonekana akiweka makubaliano.



 Picha ya Pamoja ilipigwa
 Hao wameshiriki kuweka makubaliano hayo



mazungumzo yaliendelea kati ya mkuu wa wilaya na mzee wa mila wa koo ya Wakenye