Fahari ya Serengeti

Thursday, April 26, 2018

UPANDAJI MITI SERENGETI WASHIKA KASI

 Das Serengeti Cosmas Qamara akipanda mti ikiwa ni mkakati wa wilaya hiyo kuhakikisha wanapanda miti 1.5 mil kama ilivyoagizwa na Makamu wa Rais na pia miti 100,000 agizo la mkuu wa Mkoa huo,wilaya hiyo ndiyo iliyobaki na mistu mingi kwa mkoa huo na huzalisha mkaa unatumika ndani na nje ya mkoa wa Mara kinyamera.
 Ofisa uhamiaji wilaya Henry akipanda mti
 Mkurugenzi wa Tumaini Jema akipanda mti
 DSO Molel naye ameshiriki
 Mkuu wa Gereza mahabusu akiwajibika katika utunzaji wa mazingira
 Afisa vijana hakubaki nyuma
 Wataalam mbalimbali wameshiriki
 Msisitizo wa utunzaji miti iliyopandwa ukatolewa
 Afisa habari ni miongoni mwa walioshiriki kupanda miti
Maelekezo yakatolewa

CHANJO YA SARATANI YA KIZAZI YAZINDULIWA

 Ded Serengeti Juma Hamsini amezindua chanjo ya Saratani ya mlango wa kizazi kwa watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 huku akihimiza wazazi kuruhusu watoto waweze kupata chanjo hiyo muhimu kwa afya zao.
 Nyachamba Mlaga akitoa chanjo
 Wanafunzi wa Little Flower wakiwa wamekaa wakisubiri utaratibu wa chanjo


KWAYA YA MT.MARIA YAKONGA NYOYO ZA WAUMINI

 Kwaya ya Mt.Maria Mama wa Mungu Parokia ya Mugumu Jimbo Katoliki Musoma imekonga nyoyo za waumini kwa kuimba nyimbo zenye ujumbe mzito wakati wa Misa ya Ufunguzi wa Nyumba ya Tafakuri Parokia ndogo ya Serengeti iliyoongozwa na Baba Askofu Michael Msonganzila.
Askofu ameshindwa kuficha furaha yake na kuwamwagia sifa hasa mpiga kinanda mwanamke aliyeonyesha umahiri wake na kudai katika jimbo zima mtaalam huyo wa kike anapatikana kwaya hiyo na Parokia ya Mugumu tu.


 Wanakwaya wakiwa wanafuatilia matukio mbalimbali wakati wa misa takatifu
 Wakiongoza maandamano ya kuingia kanisani kwa ajili ya kuanza misa,
 Wanakwaya wakiendelea kuimba nje ya kanisa kabla ya kufungua nyumba ya Tafakuri
 Misa inaendelea
Wanaendelea kuhubiri kwa njia ya nyimbo.

KANISA KATOLIKI KUITANGAZA HIFADHI YA SERENGETI

 Askofu wa Jimbo Katoliki Musoma Michael Msonganzila amesema kanisa hilo limeanzisha mpango mahsusi wa kutangaza hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuwa ni uumbaji wa Mungu alioufanya kwa makusudi ambao unatakiwa kuenziwa na kila mtu.
Akizindua nyumba ya Tafakuri itakayotumika kama kituo cha mapadri na waumini Parokia ndogo ya Serengeti ambayo itatumika kupumzika na kujifunza mambo mbalimbali,pia wanaandaa eneo maalum ambalo litatumiwa na makundi mbalimbali yanayokwenda na kutoka  hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupumzika eneo hilo.
 Askofu Msonganzila akifafanua jambo kwa waumini waliohudhuria ufunguzi wa nyumba hiyo.
 Askofu akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri waliohudhuria misa ya ufunguzi wa nyumba hiyo.
 Maandamano kutoka Nyumba ya Tafakuri kwenda kanisani kwa ajili ya kuanza misa takatifu

 Baraka zinatolewa
 Utepe ukakatwa
Waumini wakifuatilia matukio mbalimbali.

Tuesday, April 17, 2018

JENGA HOSPITALI KWA SH 1000 YAZIDI KUCHANJA MBUGA

 Ded Serengeti Juma Hamsini akiunga mkono Kauli mbiu ya Jenga Hospitali kwa sh 1000 kwa kutoa sh 1000,000 muda mfupi baada ya Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka kumaliza kukagua ujenzi wa hospitali hiyo na kuwasilisha ahadi yake ya Tsh 1 mil  aliyotoa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa januari mwaka huu .
Hata hivyo amewasilisha michango mingine toka kwa wadau wa maendeleo aliokutana yenye jumla ya thamani ya tsh 7 mil .
Amesisitiza wananchi hasa wakazi wa wilaya hiyo kuunga mkono Kauli mbiu hiyo kwa lengo la kupata fedha za kukamilisha baadhi ya majengo ya hospitali ambayo inategemewa kutoa huduma kwa wakazi wa mkoa huo ikiwemo watalii.

 Mambo yanazidi kuongezeka Patricia Kabaka akimuunga mama yake kutekeleza Kauli mbiu ya Jenga hospitali kwa sh 1000 kwa kuchangia sh 150,000.

 Mwenyekiti wa CCM wilaya Jakobo Bega akiwasilisha risti ya mifuko 30 ya saruji yenye thamani ya Tsh 600,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa hospitali ya wilaya.
 Mwenyekiti wa Uwt wilaya naye hakubaki nyuma
Diwani viti maalum Helana Sambayeti akichangia ujenzi wa hospitali

MWENYEKITI UWT ASHIRIKI UPANDAJI MITI

 Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka akipanda mti katika hospitali ya wilaya ya Serengeti wakazi wa ziara yake ya kukagua shughuli za ujenzi na kushiriki katika kutekeleza kauli mbiu ya Jenga Hospitali kwa sh 1000.
Upandaji wa miti katika hospitali hiyo kunalenga kuandaa mazingira mazuru kabla ya kufunguliwa mwishoni  mwa mwezi mei mwaka huu kwa ajili ya kutoa huduma kwa akina mama na watoto.
 Utunzaji mazingira




MKT UWT TAIFA AKAGUA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA SERENGETI

 Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka akiwa na viongozi mbalimbali wa wilaya ya Serengeti na Mkoa wa Mara wakati anakagua Ujenzi wa Hospitali ya wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara inayojengwa na nguvu za wananchi na wadau mbalimbali kupitia kampeini ya Jenga Hospitali kwa sh 1000.
 Mwenyekiti UWT Taifa Gaudensia Kabala akikaribishwa ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Serengeti

 Dc Serengeti Nurdin Babu akiongozana na Mwenyekiti Uwt Taifa Gaudensia Kabaka huku akimwelezea jinsi wanavyotekeleza mradi wa ujenzi wa hospitali ya wilaya kwa kupitia kauli mbiu ya Jenga  hospitali kwa sh 1000.
 Ukaguzi unaendelea



Wanaangalia baadhi ya miundo mbinu inavyoanza kuharibika kwa kuwa hospitali hiyo imeanza kujengwa mwaka 2008.

Sunday, April 8, 2018

ALIYEEZUA NYUMBA AKISHINIKIZA MKE KUHAMA AFUNGWA


Isaya Petro Mkazi wa Mtaa wa Chamoto kata ya Stendi Kuu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amehukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja kwa kosa la kuharibu mali,ametakiwa kutengeneza nyumba alizoharibu na asipatikane na kosa lolote.
Aprili 6 mwaka huu Isaya aliezua mabati nyumba mbili za familia akimshinikiza mke wake ahame ili auze mji kwa kile kinachodaiwa kuwa hana faida kwa kuwa anamzalia watoto wa kike tu.
Kutokana na ukatili huo mke na watoto wake wanaishi kwenye chumba kimoja cha kupanga kinacholipwa na wananchi wa mtaa huo.



Mariam Jakson (33)mkazi wa Mtaa wa Chamoto kata ya Stendi Kuu wilaya ya Serengeti akiwa amekaa hana la kufanya kufuatia mme wake kuezua mabati ya nyumba akimshinikiza kuhama ili auze mji kwa kuwa ana mzalia watoto wa kike.