Fahari ya Serengeti

Saturday, April 1, 2017

WADAU WAAHIDI KUSAIDIA FAMILIA YA MNANKA CHACHA

 Shirika la Social Action Trust Fund la Dar es salaam na Shirika la Jipe Moyo la Musoma wamekutana na familia ya akina Mnanka Chacha katika mtaa wa Chamoto Mugumu wilayani Serengeti ili kujua hali yao na namna ya kuwasaidia baada ya kusoma gazeti la Mwananchi la Februari 23 mwaka huu.Mnanka mtoto anayelea wadogo zake sita baada ya mama yao kufariki oktoba mwaka jana wakati anajifungua mtoto wa kumi.
Kutokana na mazingira magumu wanayoishi Mnanka alishindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza Kambarage sekondari kwa kukosa fedha za kununua mahitaji ya shule,upatikanaji wa chakula kwa ajili ya familia hiyo ,hadi wasomaji wa Gazeti la Mwananchi walipoguswa na kutoa fedha za mahitaji hayo na februari 17 mwaka huu akaanza masomo akiwa amechelewa zaidi ya mwezi mmoja.

Hata hivyo mashirika hayo ambayo yamekubaliana kuingia ubia kwa ajili ya kuwasaidia yameahidi kutekeleza ahadi hiyo mapema kwa kuwachukua watoto sita ambao watawapa matunzo na elimu,pia Mnanka atatafutiwa shule ya Bweni ili apate muda mzuri wa kusoma .
 Mnanka kulia na wadogo zake,kushoto ni diwani wa kata hiyo Charles Tunda.

 Baadhi wanajisomea mara baada ya kuamka kama walivyokutwa.

 Wadau wa SATF , Jipe Moyo na Ustawi wa Jamii wakijadiliana nje ya makazi ya akina Mnanka




0 comments:

Post a Comment