Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Nurdin Babu amewataka wajumbe wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya wafanya kazi duniani kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha.
Amesema kumekuwa na tabia ya watu kutumia vibaya fedha zinazochangwa kwa wakati wa shughuli kama hizo ,hivyo yeye hatavumilia michezo hiyo na kuwasisiiza wajumbe wa kamati ya wilaya na mkoa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake kama walivyojipangia.
"Sherehe hizi zinafanyika wilaya ya Serengeti Kimkoa lazima kama wenyeji tuhakikishe kila kitu kinakwenda vizuri,kamati ya afya fanyeni kazi yenu ili kuhakikisha maeneo yako safi ,kwa kamati ya ulinzi imarisheni ulinzi na usalama kwa kudhibiti wakorofi,"amesema.
Kamanda wa Polisi wilaya Mathew Mgema amesema polisi wanaendelea na kazi zao za kila siku za kudhibiti uharifu na kuwa wakati wa maadhimisho hayo wataongeza nguvu kwa kuwa wakati wa shughuli kama hizo wahalifu wengi hujitokeza.
0 comments:
Post a Comment