Fahari ya Serengeti

Wednesday, December 28, 2016

Matukio ya ibaada ya krismass

Askofu Mkuu wa Kanisa la Menonite la Kiinjili Tanzania Dayosisi ya Mara Naamon Kajeri akimbatiza binti aliekubali kumpokea Yesu katika ibaada maalum ya Krismasi.

Askofu Naaomi Kajeri akiwaongoza sala ya Toba vijana ambao tayari walikubali kumtumikia Mungu na kukubali kubatizwa.
Vijana sita kutoka jimbo la Musoma Kaskazini waliokubali kumpokea Yesun kuwa mwokozi wa maisha yao kwa njia ya ubatizo.
Baadhi ya Viongozi wa dini wa Kanisa la Menonite la Kiinjili Tanzania wakipongezana Mara baada ya ibaada ya Krismasi jimbo la Musoma Kaskazini.
Waumini wa Kanisa la Menonite jimbo la Musoma Kaskazini wakisalimiama mara baada ya ibaada iliyofanyika kanisani hapo.
Askofu akiwaongoza Sala wazazi waliokuwa tayari kuwaweka watoto wao wakfu katika ibaada maalum iliyofanyika Jimbo la Musoma Kaskazin.
Waumini wa kanisa la Menonite la Kiinjili Tanzania jimbo la Musoma kaskazini wakiwa wameinamisha nyuso zao kama ishara ya kuonesha utiifu mbele za Mungu katika ombi maalum.
Mama Askofu Ester Kajeri akiwasalimia waumini wa Kanisa la Menonite la kiinjili Tanzania katika ibaada ya krismasi iliyofanyika jimbo la Musoma Kaskazin
Askofu Mkuu Naamon Kajeri(katikati)na mchungaji wa Kanisa Jimbo la Musoma Kaskazini(Phares Mtatiro)wakisikiliza ujumbe wa kwaya kutoka kwaya kuu ya kanisa hilo kushoto ni Mwendesha ibaada Emmanuel Manji.
 Kikundi cha kwaya cha Musoma Kaskazini kaskazini kikiendele kutumbuiza katika ibaada maalum ya krismasi iliyoongozwa na Baba Askofu Naamon Kajeri
Askofu Naamon Kajeri  akimuwekea mikono mtoto ambae amewekwa wakfu kama ishara ya kumpa baraka katika ukuaji wake.
Mama Askofu  Ester Kajeri akisema jambo na waumini wa kanisa kanisa la Menonite la Kiinjili Tanzania katika ibaada ya Krismasi iliofanyika jimbo la Musoma Kaskazin.

0 comments:

Post a Comment