Fahari ya Serengeti

Wednesday, December 28, 2016

BUSAWE SERENGETI WAZINDUA MIRADI YA MAENDELEO

Diwani wa Kata ya Busawe wilayani Serengeti Mkoa wa Mara Ayubu Makuruma kushoto akitoa ufafanuzi wa miradi waliyotekeleza bila fedha ya serikali ikiwemo ujenzi wa Kituo cha afya na vifaa vyake chenye thamani ya zaidi ya sh 200 mil,ujenzi wa ofisi ya kijiji na kata yenye thamani ya zaidi ya sh 30 mil.miradi ya elimu na maji kwa kutumia wazawa wa kijiji na kata hiyo walioko nje ya wilaya na mkoa wa Mara,kulia ni Mkuu wa wilaya hiyo Nurdin Babu
Wazawa wa kijiji cha Busawe kata ya Busawe wakiwa pamoja na viongozi wa kijiji,kata na wilaya ya Serengeti wakijadiliana mambo mbalimbali kabla ya kazi ya kukagua miradi na harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba ya Mwalimu shule ya msingi Bisawe.
Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akiwa na viongozi wenzake wakati wakielekea kwenye chanzo cha maji katika kijiji cha Busawe.
Safari inaendelea.
Akina mama nao walikuwepo


Dk James Mataragio Mkurugenzi wa TPDC ambaye ni mzawa wa kijiji cha Busawe akihamasisha wenzake namna ya kuchangia miradi ya maendeleo ili kuwapunguzia adha wananchi .
Uzinduzi wa Ofisi ya Kijiji iliyojengwa kwa nguvu za wananchi ukifanywa na Dc Nurdin Babu
Tunakata utepe anasisitiza Dc Nurdin Babu
Kama ilivyo ada wanasaini kitabu cha wageni
Ded Serengeti Mhandisi Juma Hamsini kushoto anatoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali ambayo halmashauri yake imepanga kutekeleza kwa bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17
Dc akiongoza harambee ambapo zaidi ya sh 15 mil zilichangwa kati ya lengo la sh 24 mil kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu.

0 comments:

Post a Comment