NaibuWaziri akijadiliana na madc wa Serengeti na Bunda baada ya kuwasili eneo la Tirina wilayani Serengeti |
Ukaguzi Shambani ukiendelea
Mwenye shamba Komesha akieleza madhara aliyokwishapata toka mwaka 2014 mpaka sana ,hajawahi kuvuna wala kifuta jasho hajawahi pata licha ya kujaza fomu.
Mjadala shambani unaendelea
Hatimaye wakaendelea
Ilibidi wapitie ramani kuona ulipo mpaka wa hifadhi na makazi ya wananchi,hata hivyo imebainika licha ya kuwa mbali na hifadhi haijasaidia kutopata madhara.
Wakazi wa Singisi wakazua msafara wa waziri kwa mabango.
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Marwa Ryoba akaeleza jinsi tembo wanavyochangia umaskini wa wakazi wa wilaya hiyo kutokana na kula mazao yao,hawana chakula.
Maneno yakamwingia
Ziara ikamfikisha kwenye mji wa mkazi wa Makundusi ambaye nyumba yake iliezuliwa na tembo kisha akala chakula kilichokuwa ndani.
Mwenyekiti wa halmashauri Juma Porini akionyesha teknolojia ya kuzuia tembo iliyobuniwa na wananchi baada ya kukosa msaada wa wizara ya wanyamapori.
Askari wako imara kwa bosi wao.
Dc Nurdin Babu akasema wilaya imeishawasilisha taarifa kwa Mkuu wa Mkoa kuomba chakula cha msaada maana wakulima wamelima lakini hawavuni sababu ya tembo
Afisa wanyamapori wilaya John Lendayan akitoa taarifa ya madhara ya tembo na mikakati ya wilaya,hata hivyo amesema hali ni mbaya kunatakiwa mikakati ya haraka ili kunusuru wananchi.
Ziara ikawafikisha ofisi ya Senapa Fort Ikoma iliyoungua moto
Hatimaye wakapeana mikono ya kwa heri baada ya kuhitimisha ziara.
Wakati wa maswali waandishi hawakusita kumuuliza naibu waziri ,kwanini wanatenga fedha za kulipa waliokufa,kujeruhiwa na mazao badala ya kuzielekeza kwenye ulinzi,amesema wizara itafanyia kazi eneo hilo kwenye mipango yake.
Hatimaye safari ya kuelekea Mwanza ikaanza.