Fahari ya Serengeti

Saturday, April 2, 2016

KAMPEINI YA UPANDAJI MITI ENEO LA GEREZA MAHABUSU MUGUMU SERENGETI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Naomi Nnko akipanda mti katika eneo la Gereza Mahabusu,jumla ya miti 375 imepandwa ,wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2015/16 imepewa lengo la kupanda miti 1.5 milioni ,hadi sasa miti zaidi ya laki nane imepandwa.
 Mkuu wa wilaya hiyo Ally Mafutah wa pili kutoka kulia akijadiliana na baadhi ya maafisa wa halmashauri hiyo na hoteli ya Four Season Safari's mara baada ya kupanda miti.

 Kazi inakwenda ikiongezeka kama inavyoonekana hapo ,Mkurugenzi akitekeleza jukumu lake,HAPA KAZI TU.
 Dc akiongoza baadhi ya wataalam wengine kupanda miti katika eneo hilo,kazi iliyokutanisha wadau mbalimbali kama Alliance One Tobacco ,Setco na Four Season Safari's .

 Mkuu wa wilaya akijadiliana na maafisa wa gereza mahabusu Mugumu Serengeti mara baada ya kukamilisha kazi ya upandaji miti kwenye eneo hilo.
 Mkuu wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai wilaya hiyo naye alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika zoezi hilo muhimu
Mshauri wa Mgambo akiwa anapanda mti



 Kazi na dawa mara baada ya kumaliza kazi hiyo walipata chai iliyoandaliwa na Four Season Lodge


Hilo ni zao la chuo cha utalii (SETCO)

0 comments:

Post a Comment