Fahari ya Serengeti

Saturday, March 26, 2016

ZIARA YA MAFUNZO WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI GIBASO -TARIME NA MERENFA -SERENGETU FOUR SEASON SAFARI'S LTD YAWAKUNA WANAFUNZI

Viongozi wa hifadhiya Taifa ya Serengeti,hoteli ya Four Season Safari's Ltd wakiwa pamoja na wanafunzi sita na mwalimu kutoka shule ya Msingi Gibaso wilaya ya Tarime ambao walifanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza mwaka 2015,Hifadhi ya Senapa kwa kushirikiana na Hoteli hiyo wameanzisha mpango wa kuwapa motisha wanafunzi wa shule zilizoko pembezoni mwa hifadhi hiyo kwa wilaya za Tarime na Serengeti kufanya ziara ya mafunzo ili kuongeza ushindani.
Wanafunzi hao wakiwa katika chumba maalum cha kujifunzia,(maktaba ya watoto)hotelini hapo wakichora baadhi ya wanyama pamoja na kujifunza mambo mbalimbali lengo ni kuwajengea uwezo wa kutambua fursa zinazowazunguka na namna ya kutunza maliasili zetu kwa kuwa zina faida .
Wanajifunza mzunguko wa Nyumbu kutoka Masai Mara na kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuvuka Mto Mara,kisha kuelekea kusini kwa ajili ya kuzaa


Michoro inaendelea

Walifika maeneo mbalimbali
Hao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Merenga wilaya ya Serengeti wakiwa pamoja na viongozi wa Senapa na hoteli hiyo mara baada ya kuwasilia hapo kwa ajili ya kuanza ziara ya mafunzo.

Kazi na dawa hapa wanaweka afya vizuri ili waweze kuendelea na utalii

Mmoja wa walinzi katika hoteli hiyo maarufu kama Masai akiwaeleza mambo mbalimbali yanayovutia yanayopatikana katika hoteli hiyo ya kitalii









Hapo anatafutwa Bingwa wa mchoro ,wawili kati yao walipata zawadi kwa kuchora vizuri baadhi ya wanyama
Picha ya Pamoja ilipigwa
Wanachagua zawadi mbalimbali baada ya kumaliza ziara ya mafunzo

Kila mmoja alichagua alichoona kinafaa

0 comments:

Post a Comment