Fahari ya Serengeti

Sunday, March 27, 2016

WANANCHI WAJITOKEZA KUFANYA USAFI MAKABURINI MUGUMU

 Baadhi ya wakazi wa mji wa Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakiendelea na zoezi la usafi wa makaburi,ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya usafi
 Eneo la makaburi lilikuwa limegeuka vichaka vya waharifu,kupitia mkakati huo itasaidia eneo hilo kuwa safi
 Baadhi ya wakazi wa mji wa Mugumu wakiwa wamepumzika juu ya makaburi baada ya kufanya kazi ya kufyeka eneo hilo.
 Kazi ya kufyeka inaendelea

 Hapa kazi tu kila mmoja anaonekana anaendelea na kazi

 Kazi hiyo ilijumuisha watu wa rika mbalimbali




 Hata wanawake walishiriki kufanya usafi hamsini kwa hamsini .
 Hamsini kwa hamsini ilikuwepo



MATUKIO YA MKESHA WA PASAKA PAROKIA YA MUGUMU SERENGETI

 Kwaya ya Mtakatifu wa Asizi Parokia ya Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wakihubiri kwa njia ya nyimbo wakati wa misa ya mkesha wa Pasaka.
 Paroko wa kanisa Katoliki ya Mugumu Alois Magabe wakati wa ibada ya mkesha wa pasaka
 Wanakwaya wakati wa maombi

 Hongera umebatizwa anaonekana katekista Anthony Marwa anampongeza mmoja wa waumini waliobatiwa katika ibada hiyo.
 Padri Japhet Mwaya akiwa na mshumaa wa pasaka
 Hongera kwa ubatizo


 Mzee Japhet Mwiturubani (99)alibatizwa na kisha kufunga ndoa na mke wake






Saturday, March 26, 2016

ZIARA YA MAFUNZO WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI GIBASO -TARIME NA MERENFA -SERENGETU FOUR SEASON SAFARI'S LTD YAWAKUNA WANAFUNZI

Viongozi wa hifadhiya Taifa ya Serengeti,hoteli ya Four Season Safari's Ltd wakiwa pamoja na wanafunzi sita na mwalimu kutoka shule ya Msingi Gibaso wilaya ya Tarime ambao walifanya vizuri kwenye mtihani wa kumaliza mwaka 2015,Hifadhi ya Senapa kwa kushirikiana na Hoteli hiyo wameanzisha mpango wa kuwapa motisha wanafunzi wa shule zilizoko pembezoni mwa hifadhi hiyo kwa wilaya za Tarime na Serengeti kufanya ziara ya mafunzo ili kuongeza ushindani.
Wanafunzi hao wakiwa katika chumba maalum cha kujifunzia,(maktaba ya watoto)hotelini hapo wakichora baadhi ya wanyama pamoja na kujifunza mambo mbalimbali lengo ni kuwajengea uwezo wa kutambua fursa zinazowazunguka na namna ya kutunza maliasili zetu kwa kuwa zina faida .
Wanajifunza mzunguko wa Nyumbu kutoka Masai Mara na kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kuvuka Mto Mara,kisha kuelekea kusini kwa ajili ya kuzaa


Michoro inaendelea

Walifika maeneo mbalimbali
Hao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Merenga wilaya ya Serengeti wakiwa pamoja na viongozi wa Senapa na hoteli hiyo mara baada ya kuwasilia hapo kwa ajili ya kuanza ziara ya mafunzo.

Kazi na dawa hapa wanaweka afya vizuri ili waweze kuendelea na utalii

Mmoja wa walinzi katika hoteli hiyo maarufu kama Masai akiwaeleza mambo mbalimbali yanayovutia yanayopatikana katika hoteli hiyo ya kitalii









Hapo anatafutwa Bingwa wa mchoro ,wawili kati yao walipata zawadi kwa kuchora vizuri baadhi ya wanyama
Picha ya Pamoja ilipigwa
Wanachagua zawadi mbalimbali baada ya kumaliza ziara ya mafunzo

Kila mmoja alichagua alichoona kinafaa