Fahari ya Serengeti

Tuesday, February 2, 2016

SINGITA GRUMETI RESERVES NA GRUMETI FUND WAIKUMBUKA MAHAKAMA YA WILAYA KWA VIFAA VYA KISASA


 KAMPUNI YAISAIDIA MAHAKAMA KOMPUTA,
Na Serengeti Media Centre(SMC)

Mahakama ya Hakimu Mkazi wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara imetakiwa
kusikiliza kesi kwa haraka na kutoa nakala za hukumu kwa muda mfupi
ili kupunguza malalamiko ya jamii.

Katibu Tawala wilaya hiyo Cosmas Qamara akikabidhi komputa ya kisasa
kwa hakimu wa mahakama hiyo iliyotolewa na Kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Grumeti Fund yenye thamani ya zaidi y ash 3.8 milioni ,ili kusaidiauharakishaji wa utoaji haki kwa njia ya kisasa ,alisema msaada huo unatakiwa kusaidia kuongeza ufanisi katika mhimili huo muhimu.

Alisema ili kwenda na kasi ya utendaji wa serikali ,kesi zinatakiwa
kushughulikiwa kwa muda mfupi na kutoa haki ili kuwapunguzia mizunguko
na gharama wananchi ,ikiwemo suala la  ucheleweshaji wa nakala za
hukumu ambalo limekuwa kero kubwa kwa jamii.

“Huu ni mwendelezo wa Kampuni ya Singita  Grumeti Reserves na Grumeti Fund kutoa misaada ili kuboresha huduma za Jamii ,wamesaidia sana nyanja za Elimu,Afya,Maji,Barabara,Polisi,Wajasiriamali   na sasa Mahakama ,lengo ni kuhakikisha jamii inapata huduma bora, na kwa wakati,tunategemea kesi zitaenda kwa haraka maana kumbukumbu zitatunzwa  kisasa ,”alisema.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Juma Porini alisema kazi inayofanywa na
Kampuni hiyo ni kubwa na kama wawekezaji waliomo wilayani humo
wangetimiza wajibu wao kama hiyo kampuni wilaya ingesonga mbele
kimaendeleo.

Hata hivyo aliwataka waendesha mashitaka wabadilike kwa kuwa
wanachangia kuchelewa kwa kesi,”watu wanakaa miaka minne mahabusu kisa ushahidi haujakamilika,mwisho wa hukumu wanaachiwa wakati wamepoteza muda wao gerezani,kwa msaada huo tunategemea mabadiliko makubwa kiutendaji kwa kuwa nyaraka zitatunzwa na kupatikana kwa wakati,”alisema.

Akitoa ufafanuzi kabla ya kukabidhi  msaada huo kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Fund , Meneja Mahusiano wa kampuni hiyo  Ami Seki alisema lengo ni kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma kwa jamii.

“Kampuni ilipopata maombi ya Mahakama kuwa inakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa komputa na kuchangia  kumbukumbu nyingi kupotea na kusababisha kesi kuchelewa..pia hawawezi kutoa nakala kwa wakati ,tukaamua kutoa msaada huu ,lengo ni kuhakikisha haki ionekane
inatendeka kwa wakati,”alisema.

Mapema Hakimu wa Mahakama hiyo Emmanuel Ismaeli Ngaile alisema kupitia msaada huo watakuwa wanatoa nakala za hukumu ndani ya wiki moja ,ili kuwawezesha wananchi kutafuta haki kadri ya mahitaji yao.

“Kampuni ya Singita Grumeti Reserves na Fund imefanya tendo kubwa kwa mahakama ,maana tulikuwa na mapungufu makubwa ya utoaji wa nakala za hukumu,hii ni safari ya kuifanya mahakama ifanye kazi kisasa kwa kuwasiliana kwa njia ya mtandao,”alisema.

Baadhi ya mahabusu na wananchi waliokuwa mahakamani hapo walisema
msongamano mkubwa wa mahabusu gerezani unachangiwa na ucheleweshaji wa kesi,hivyo mahakama na waendesha mashitaka wautumie vema msaada huo kuipunguzia serikali gharama za kuwahudumia mahabusu.
Mwisho.
























1 comment:

  1. Mmmh!nikiwa na kesi ninayomshyaki huyo mwekezaji aliyetoa msaada wa kompyuta kwa mahakama je haki itatendeka?

    ReplyDelete