WAZIRI wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe akipata taarifa kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa Ndege kwa ajili ya doria iliyokabidhiwa na Balozi wa Ujermani Egon Konchanke aliyeko katikati,wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAWA Martin Loiboki na Mkurugenzi wa Tanapa Allan Kijazi.
Balozi wa Ujermani Egon Konchanke akitoa ufafanuzi wa msaada huo wa ndege mbili moja itatumiwa maeneo ya Selous kwa ajili ya kupambana na Ujangili.
Ndege hiyo aina ya Aviat Air Craft Husky A-Ic inabeba watu wawili na inatumia galoni 5 za mafuta kwa saa moja na inagharimu dola 200,000 za Kimarekani.
Rubani wa Ndege hiyo anasema inauwezo wa kwenda kilometa 5 toka chini ,inabeba galoni 50 na ina uwezo wa kuruka saa 10 na haina kelele,inapiga picha matuki yote ya uhalifu na kutuma taarifa kwa askari walioko chini .imetengenezwa mwaka 2015 Amerika.
Simba wakiwa wamejituliza pembeni mwa barabara ya kuelekea lango la Naabi
Simba akiwa amekaa mkao wa kutafuta mawindo,huku Punda milia wakawa wanamwangalia kwa tahadhari