Fahari ya Serengeti

Tuesday, February 3, 2015

WATOA MISAADA YAO BINAFSI KWA WASICHANA WALIOKIMBIA KUKEKETWA

WAJITOKEA KUSAIDIA WASICHANA WALIOKIMBIA KUKEKETWA
Serengeti:Wafanyakazi wawili wa benki ya Nmb tawi la Mugumu wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara wametoa msaada wa nguo 117 zenye Thamani ya sh 234000 kwa wasichana 38 waliokimbia kukeketwa mwaka Jana wanaoishi  nyumba salama.

Mwaka Jana wasichana 134 walikimbia kukeketwa na kuhifadhiwa katika nyumba salama iliyo chini ya kanisa la Anglikana dayosisi ya Mara ,kati yao 38 hawakurudi kwao kwa hofu ya kufanyiwa ukatili,na baadhi ya wazazi wakigoma kuwalipia karo kwa madai ya kutokukeketwa.

Liliani Magiro na Beatrice Mbuya wakikabidhi msaada huo kwa mratibu wa mradi wa nyumba salama Rhobi Samweli walisema wameguswa na tatizo la hao wasichana ambao wamekuwa Mfano kwa wengine kwa kukataa kukeketwa kwa kutambua Madhara yake,

"Msaada huu tumetoa sisi  wenyewe wala si benki,kupitia vyombo vya habari tuliguswa na tatizo lao kwa kuwa tulijua wakati wanatoroka hawakuweza kuchukua nguo zao.....hivyo watakuwa na upungufu wa mavazi,tukaamua kuja Kutoa msaada huu"alisema Mbuya.

Walisema Kuwa wataendelea kusaidia kadri watakavyofanikiwa kupata ili kuwawezesha wasichana hao kufikia malengo ya maisha yao kwa kuwa uamzi waliouchukua ni dalili Kuwa wanajitambua .

"Ninachowaomba ni kujitahidi kusoma kwa bidii ili elimu hiyo waitumie kuwasaidia na wengine kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia hasa matendo ya ukeketaji ambao una Madhara makubwa kiafya"alisema Magiro.

Akipokea msaada huo mratibu wa nyumba salama Samweli alisema tatizo lililowakuta wasichana hao ni matokeo ya mfumo unaomkandamiza mtoto wa kike kwa Kuwa wazee wa mila wanalazimisha ukeketaji kwa msingi wa kupata fedha kwa Kuwa wao hawapati uchungu.

Aliomba Wadau mbalimbali kujitokeza kuwasaidia kwa mambo mbalimbali"hapa wanahitaji msaada ,tumeanzisha kozi mbalimbali kwa wale waliokuwa Shule wazazi wamegoma kuwasomesha tunawalipia karo...wengine wanasoma kozi mbalimbali ikiwemo ushonaji na komputa ,"alisema,

Nao wasichana hao walishukuru kwa msaada huku wakiomba Watu mbalimbali kuwasaidia ili waweze kufikia Malengo yao ya masomo,kwa  huku wakiitaka  serikali kusimamia sheria dhidi ya wazazi wasio timiza  wajibu wao kwa kuwashughulikia baadhi wazazi wanavunja sheria.

Mwisho.

 LILIAN NA BEATRICE WAFANYAKAZI WA BENKI YA NMB TAWI LA MUGUMU WILAYA YA SERENGETI WAKIWA NA WASICHANA WALIOKIMBIA KUKEKETWA WALIOKO NYUMBA SALAMA KANISA LA ANGLIKANA MUGUMU DAYOSISI YA MARA BAADA YA KUTOA MISAADA YAO BINAFSI YA NGUO.

 WAKIKABIDHI MISAADA YAO BINAFSI KWA MRATIBU WA NYUMBA SALAMA RHOBI SAMWELI

 RHOBI SAMWELI AKIANDIKA BARUA YA KUWASHUKURU KWA MOYO WAO WA KUJITOA NA KUWASAIDIA WASICHANA HAO .




0 comments:

Post a Comment