Fahari ya Serengeti

Sunday, February 15, 2015

PICHA NA HABARI ZA MATUKIO YA MWANAMKE ALIYEDAIWA KUPOTEA KATIKA MAZINGIRA TATA ROBANDA-SERENGETI

Feb.16,2015.
Serengeti:Mwanamke aliyepotea feb 9,mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha katika kijiji cha Ikoma robanda wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amepatikana ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti akiwa mzima.
Kupatikana kwa Nyangi Sagoche(30)kumethibitishwa na uongozi wa kijiji,polisi na mganga mfawidhi wa zahanati ya Robanda alikolazwa kwa matibabu,kumekuja huku wakazi wawili wa kijiji hicho wakiwa wamelazwa hospitali Teule ya wilaya ya Nyerere baada ya kupigwa na wananchi wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina kijijini hapo.
Akiongea na Blog hii kwa kugugumia  kutokana na kudhoofika wakati amelazwa katika zahanati ya Robanda Nyangi alisema ,aliokotwa  na dreva wa gari la Kampuni ya Thomson pembeni mwa barabara lililokuwa na wageni ,ikiwa ni siku ya sita akizunguka ndani ya hifadhi hiyo yenye wanyama wakali bila kujua alivyofika huko.
“Sijui nilifikaje huko,maana nakumbuka februari 9 usiku nikitoka senta kwenda nyumbani niliitwa na mzee mmoja anayeishi kitongoji cha Mereshi anajishughulisha na kucheza ngoma za asili…akanilazimisha kwenda kunywa pombe,nilikataa akasema umenikatalia haya,hapo ndipo nilipoteza fahamu na sijui ilikuwaje hadi leo(jana)nilipookotwa”alisema.
Alisema kwa siku zote sita hakuwahi kula wala kunywa lakini akawa ni mtu wa kutembea porini huku wanyama wakali kama Simba ,tembo ,nyati  na Fisi akipishana nao,usiku  akilala kwenye miti,”ramani ya nyumbani nikawa siijui,hata sijui nilifikaje pembeni mwa barabara nikaa chini ya mti hadi nilipookotwa,si tukio la kawaida najua lililonikuta”alisema bila kufafanua.
Kwa kipindi chote alikuwa akilalamika njaa na kuwa mwili wake umejaa miiba,hata hivyo licha yakutembea porini bila viatu , hakuwa na jeraha la kuchomwa na miiba hali iliyozidisha maswali kutoka kwa wananchi.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo Christopher Charles alisema Nyangi alifikishwa kituoni hapo akiwa amedhoofika sana na kuwekewa maji kwa muda mfupi chupa tatu zikawa zimeisha na kuomba kukojoa ikiwa ni dalili kuwa alikuwa ameishiwa maji.
“Kwa kwa mwanamke akikaa siku saba bila kula ama kunywa chochote anaweza kufa,huyu alikuwa akitumia akiba ya chakula chake mwilini,na kilikuwa kinaelekea kuisha kabisa ,tatizo alilonalo ni hilo tu,maana akili iko vizuri,hana jeraha sehemu yoyote katika mwili wake”alisema.
Akizungumzia tukio hilo mme wake Marekanyi Charles(31)alisema tukio hilo si la kawaida kwa kuwa amepatikana ikiwa ni siku moja tu baada ya watu wanadaiwa kujihusisha na mambo ya ushirikina kutajwa na kuadhibiwa ,wengi wakirudisha mikoba yao,miongoni mwao akiwemo baba yake mzazi.
“Huyu mwanamke tulikuwa tumetengana naye kwa muda,lakini akitoka hapa hospitali itabidi arudi nyumbani tuishi na tulee watoto wetu watatu,maana nimegundua kuwa huyu mwanamke alikuwa anazongwa na mambo yasiyo ya kawaida”alisema.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Itabe Nkiri alisema kwa muda wa siku nne shughuli mbalimbali za uchumi kwa ajili ya msako wa huyo mwanamke ,hivyo kupatikana kwake kunaleta nafuu kijijini na kuomba jamii iachane na imani za kishirikina bali wamrudie Mungu.
“Mambo ya ushirikina yanashika kasi sana hapa maana februari 7 kijana mmoja Matiko Mkeya alipotea na tarehe 8  mwezi huu akapatikana akiwa amefungwa sanda….watu waliotajwa na jamii waliadhibiwa,siku ,moja tu likatokea hili kuna kila sababu ya jamii ikae iweze kuonyana maana madhara yake ni makubwa ,watu kuhasimiana na kupoteza muda wa kuzalisha mali”alisema.
Mwenyekiti wa Jamii ya Waikoma kijiji cha Robanda Masauta Shitabara alisema tukio la kupatikana kwa Nyangi akiwa hana jeraha wala michubuko kilometa 16 ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti linazua maswali na kudai akipatana ahueni wataitisha kikao ili awaambie wananchi kilichotokea kwa kuwa kumeibuka matukio yasiyo ya kawaidia kijijini hapo.
“Amepatikana siku tuliyotangaza mapumziko ,ikiwa siku moja tu watu 19 wamebanwa na jamii kutokana na kujihusisha na vitendo vya kishirikina,wapo waliorudisha mikoba yao ikiwemo mafuta ya mtu,ngozi ya mtoto,na dawa mbalimbali,na baada ya kupatikana kwa huyu katika kikao cha jamii tutaelezana mambo mengi”alisema.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia ndogo ya Fort Medard Chegere akimwombea Nyangi hapo Zahanati aliwataka wamrudie Mungu wa kweli waache kuabudu Miungu kwa kuwa hayo ndiyo matokeo yake,matukio hayo yawe fundisho kwao.
Wakati huo huo katika kijiji cha Miseke kata ya Manchira wilayani hapa alipatikana mwanamke mmoja akiwa hawezi kuzungumza kwa madai kuwa amekatwa ulimi ,huku wengine wakidai ni msukule ikiwa haijulikani alikotokea.
Mchungaji wa kanisa la Anglikana Miseke Sedekia Chikumbiro na Mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Mturi Mtumbe walisema baada ya kumchunguza walikuta ulimi umekatwa na ndiyo maana hawezi kuongea,kwa kuwa akili yake iko vizuri kwa kuwa akiona watu anaona aibu lakini hawezi kuzungumza kwa ufasaha.
Kamanda wa polisi wilaya ya Serengeti Pius Mboko aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi ,badala yake matukio yote yashughulikiwe kwa misingi ya kuheshimu misingi ya Haki za Binadamu.
Mwisho.

 NYANGI MKAZIWA KIJIJI CHA ROBANDA  WILAYA YA SERENGETI ALIYEPOTEA JANUARI 9 USIKU AKITOKA KWENYE KILABU CHA POMBE ,HATA VIVYO MSAKO WA JAMII ULIAMBULIA MALAPA,CHUPI .JUHUDI ZA KUMSAKA KIJIJINI NA PORINI KWA MUDA WA SIKU TANO HAZIKUZAA MATUNDA HADI FEB 15 MAJIRA YA ASUBUHI ALIPOKUTWA NA GARI LILILOKUWA LIMEBEBA WAGENI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI AMEKAA,HAPO YUKO KITUO CHA AFYA ROBANDA AKIPATA HUDUMA ,KWA MJIBU WA MGANGA MFAWIDHI CHRISTOPHER CHARLES AMESEMA MWANAMKE HUYO HANA JERAHA LOLOTE BALI ALIKUWA NA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU KUTOKANA NA KUTOKULA KWA MUDA MREFU.
 ANAPATA HUDUMA
 NDUGU ZAKE NA WAKE ZA SHEMEJI ZAKE WAKIMHUDUMIA
 MGANGA MFAWIDHI WA KITUO AKIMHUDUMIA
 ANASINDIKIZWA KWENDA KUJISAIDIA
 ANANYWESHWA UJI



 PADRI MEDARD CHEGERE PAROKO WA PAROKIA NDOGO YA FORT AKIMWOMBEA


MAOMBI YANAENDE;EA

0 comments:

Post a Comment