Fahari ya Serengeti

Saturday, April 9, 2016

MKUU WA MKOA WA MARA ATOA SALAMU NZITO KWA WATUMISHI MAFISADI,WALA RUSHWA NA WASIWAJIBIKA

Mkuu wa Mkoa wa Mara Magesa Mulongo akiongozana na Mkuu wa wilaya ya Serengeti Ally Mafutah ktkt na kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri Victor Rutonesha wakati wanaelekea ukumbi wa Mkutano wa halmashauri  ya wilaya ya Serengeti
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Serengeti wakiwa wamesimama wakisubiri Mkuu wa Mkoa ashule tayari kwa kuelekea uwanjani
Wanajadiliana
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Serengeti Victor Rutonesha akitoa maelezo mafupi kabla ya kumkaribisha dc kwa ajili ya kutoa taarifa ya wilaya.

Watumishi wa halmashauri,taasisi za serikali na zisizo za serikali,wadau wa maendeleo wakimsikiliza Rc Mara wakati wa kikao chake cha kwanza cha utambulisho kilichokwenda na maagizo mazito kwa watendaji na madiwani
Wanafuatilia
Wanafuatilia mjadala

DC akitoa taarifa ya wilaya
Kila mmoja alilazimika kuandika mambo yanayomgusa ili aweze kuchukua hatua kwa kuwa utendaji wa mazoea hauna nafasi tena .

RC mara akitoa maagizo kwa watendaji,wawakilishi na dau wengine
Hata hawa walikuwepo

Saturday, April 2, 2016

KAMPEINI YA UPANDAJI MITI ENEO LA GEREZA MAHABUSU MUGUMU SERENGETI

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara Naomi Nnko akipanda mti katika eneo la Gereza Mahabusu,jumla ya miti 375 imepandwa ,wilaya hiyo kwa kipindi cha mwaka 2015/16 imepewa lengo la kupanda miti 1.5 milioni ,hadi sasa miti zaidi ya laki nane imepandwa.
 Mkuu wa wilaya hiyo Ally Mafutah wa pili kutoka kulia akijadiliana na baadhi ya maafisa wa halmashauri hiyo na hoteli ya Four Season Safari's mara baada ya kupanda miti.

 Kazi inakwenda ikiongezeka kama inavyoonekana hapo ,Mkurugenzi akitekeleza jukumu lake,HAPA KAZI TU.
 Dc akiongoza baadhi ya wataalam wengine kupanda miti katika eneo hilo,kazi iliyokutanisha wadau mbalimbali kama Alliance One Tobacco ,Setco na Four Season Safari's .

 Mkuu wa wilaya akijadiliana na maafisa wa gereza mahabusu Mugumu Serengeti mara baada ya kukamilisha kazi ya upandaji miti kwenye eneo hilo.
 Mkuu wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai wilaya hiyo naye alikuwa miongoni mwa walioshiriki katika zoezi hilo muhimu
Mshauri wa Mgambo akiwa anapanda mti



 Kazi na dawa mara baada ya kumaliza kazi hiyo walipata chai iliyoandaliwa na Four Season Lodge


Hilo ni zao la chuo cha utalii (SETCO)