Fahari ya Serengeti

Sunday, October 19, 2014

WANANCHI WADAI UJANGILI UTAKWISHA KWA KUSHIRIKISHWA SI KUNUNUA SILAHA NA HELKOPITA

 WAKAZI WA KIJIJI CHA MISEKE KATA YA MANCHIRA WILAYA YA SERENGETI WAKIWA KWENYE  MKUTANO WA KUJADILI MIKAKATI YA KJUDHIBITI UJANGILI WA TEMBO,WAMEIOMBA SERIKALI ISIWE YA KUTOA MATAMKO BILA KUFANYA UTAFITI KWA NINI UJANGILI ULIPUNGUA MIAKA YA 80-90 NA KWASASA KWA NINI UMEONGEZEKA,WAFIKE VIJIJI WAAMBIWE,
 TEMBO AKILA MAZAO ASKARI HAWAFIKI,AKIUAWA TEMBO MAGARI HUJAA NA ASKARI,MAHUSIANO YA JAMII NA WAHIFADHI YANATAKIWA KUJENGWA KWA KUTATUA MATATIZO KWA PANDE ZOTE,WANANCHI WANADAI
 TUNADILIANA
 MAJADILIANO YANAENDELEA
 WANAWAKE WAKIJADILIANA KUHUSU TATIZO LA UJANGILI,PAMOJA NA KUDAI HAMSINI KWA HAMSINI HAWAWEZI KUJADILI MASUALA MBELE YA WANAUME.
 WANANCHI NDIYO WAHIFADHI WA KWANZA LAKINI MATATIZO YA UJANGILI YANAZUNGUMZWA MAREKANI,LONDON WAO HAWAFIKIWI ILI KUWEKA MIKAKATI YA PAMOJA NAMNA YA KUKABILIANA NA UJANGILI.
SERENGETI MEDIA CENTRE ILIPOKUTANA NA WANANCHI WAIISHIO KANDO KANDO YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI,MAPORI YA AKIBA NA HIFADHI YA JAMII ILIWAWEZESHA KUJUA NINI KINATAKIWA KUFANYIKA ILI KUKABILIANA NA WIMBI LA UJANGILI WA TEMBO KATIKA MAENEO YALIYOHIFADHIWA,USHIRIKISHWAJI JAMII NDIYO SILAHA YA KWANZA IMEELEZWA.

0 comments:

Post a Comment