Wednesday, August 6, 2014
TEMBO WAONGEZEKA MAPORI YA AKIBA YA IKORONGO/GURUMETI
Tembo
Agosti,2014
Wakati Tembo katika mapori mengi ya akiba wakidaiwa
kupungua,hali ni tofauti kwa Mapori ya akiba ya Ikorongo na Gurumeti wilayani
Serengeti wameongezeka kutoka 355 hadi 1,236 kwa kipindi cha mwaka miaka kumi.
Ongezeko hilo ni sawa na tembo 84 kwa kila mwaka
linachangiwa na ulinzi madhubuti wa askari wa mapori hayo kwa kushirikiana na
Kampuni ya Gurumeti Reserves ambao wamekodi vitalu hivyo.
Mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahamod Mugimwa
hivi karibuni ,Meneja wa Mapori hayo
Nollasco Ngowe akitoa taarifa kuhusu mapori hayo alisema ,walifanya sensa mwaka
2003 wakapata tembo 355 na mwaka 2013 ikiwa ni baada ya miaka kumi wamepata
tembo 1,236,ikiwa tofauti na mapori mengine ambayo idadi hushuka.
“Pamoja na changamoto tulizonazo za upungufu wa askari
,magari na wingi wa vituo…migogoro ya tembo na wakulima….bado ulinzi umekuwa
madhubuti hali ambayo inasaidia kudhibiti majangili”alisema.
Meneja huyo alisema ili kuimarisha ulinzi katika mapori hayo
aliomba wizara kuwaongezea askari na magari,kwa kuwa askari waliopo ni
wachache kulingana na kazi za
ulinzi,kufukuza tembo,doria na kuongoza watalii wa kupiga picha katika mapori
hayo.
Kuhusu uharibifu wa mazao alisema hilo ni tatizo kubwa kwa
vijiji vinavyowazunguka ,”kwa kushirikiana na Kampuni ya Gurumeti Fund kama
serikali itatoa kibali wako tayari kutumia risasi za pilipili zinazopigwa
usoni….inapomuwasha tembo anakimbia na hataweza kurudi eneo hilo…pia kutumia
bunduki aina shortgun….kuna tafiti zimeonyesha njia hiyo imesaidia”alisema.
Alibainisha kuwa baadhi ya tembo wamekimbia Masai Mara na
kuingia Tanzania ambao huenda wanachangia kuingia kwenye mashamba kwa
wingi,”hilo tunalitafiti,lakini pia wananchi kutokufuata sheria inayowataka walime
mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi,”alisisitiza.
Kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na utalii wa kupiga
picha alisema wageni 4020 waliingia na kufanikiwa kukusanya dola za Kimarekani
1,195,540 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013-14.
Akizungumzia maombi hayo Naibu waziri Mgimwa alisema kwa kuwa wanatarajia Mamlaka ya Wanyama Pori
kuanza wakati wowote wizara
imefanya usaili kwa askari 495,hivyo
wapo watakaopelekwa kwenye mapori hayo kuimarisha ulinzi.
Kwa suala la udhibiti wa tembo wanaovamia mashamba,aliwataka
waachane na njia zingine za risasi za pilipili kwa kuwa haina faida kwa
jamii,bali watumie njia ya nyuki yenye faida kwa jamii”imebainika nyuki ni njia
nzuri ya kudhibiti tembo….wananchi wanapata asali…huku wakidhibiti tembo,hiyo
ni faida”alibainisha.
Alisema wizara iko tayari kusaidia wananchi kwa kutumia
mizinga ya udongo ambayo inalenga kuhifadhi zaidi mazingira,na kumtaka
Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha vikundi ama mashirika
yasiyo ya kiserikali yanahusika ili mtandao wa mizinga uzibe kote.
Hata hivyo alitaka waangalie kati ya mabilioni
yanayokusanywa kiasi gani kinarudi kwa wananchi ili waone faida za uhifadhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri hiyo Goody Pamba alisema kwa kushirikiana na shirika la Sederec
,Gurumeti Fund wameanza kutumia njia hiyo kwa baadhi ya vi