Na Mussa Juma,
Mwananchi
Posted Alhamisi,Januari8 2015
KWA
UFUPI
NI ile yenye urefu wa
kilomita 421 iliyopaswa kujengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya Sh648
bilioni.
Arusha, Ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami
kutoka Mto wa Mbu, wilayani Monduli, Mkoa wa Arusha hadi Nata, wilayani
Serengeti, Mkoa wa Mara umekwama baada ya Serikali kushindwa kutoa fedha kama
ilivyoahidi awali.
Serikali iliahidi
kujenga barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 421 kwa gharama ya Sh648 bilioni,
huku eneo linalokatiza ndani ya hifadhi lenye kilomita 53, likitarajiwa
kujengwa kwa changarawe.
Meneja wa Wakala wa
Barabara Mkoa wa Arusha, Deusdedit Kakoko alisema pamoja na kwamba Serikali
haijatoa fedha hadi sasa, ahadi ya kujenga barabara hiyo iko palepale.
Kauli hiyo iliungwa
mkono na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Jowika Kasunga wakati akizungumza kwenye
Kikao cha Bodi ya Barabara Arusha kilichofanyika juzi.
“Ni kweli ujenzi wa
barabara haujaanza, lakini ahadi ya kuijenga iko palepale, kinachosubiriwa ni
fedha kutoka Serikali Kuu,” alisema Kasunga.
Awali, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Ngorongoro, Elias Ngolisa alihoji lini barabara hiyo itaanza
kujengwa kutokana na umuhimu wake.
Ngolisa aliitaka
Serikali kueleza kwa nini haijatoa kiasi cha fedha za awali za ujenzi huo,
kiasi cha Sh7 bilioni.
“Pamoja na fedha hizo
kutotolewa hadi sasa, bado kiasi hicho ni kidogo, labda kitumike kukarabati na
siyo kujenga,” alisema.
Ahadi ya ujenzi huo
ilitolewa na Rais Jakaya Kikwete ili kuwapunguzia usumbufu wakazi wa Arusha na
Mara kutokana na mikoa hiyo kutounganishwa kwa barabara ya lami.
0 comments:
Post a Comment