Ng'ombe wakitolewa kambi la Lamai
Vibarua wa kampuni ya Isaack and Son's wakilima zao la alzeti huku wakiongozwa kwa ngoma kazi hiyo inadaiwa kufanywa na kabila la wasukuma,shamba hilo lilo katika maeneo ya Gibaso wilayani Tarime,hata hivyo linadaiwa kuwa na mgogoro kati ya kampuni hiyo na wakazi wa kijiji cha Gibaso.
Kazi na dawa ,ngoma hiyo inadaiwa huwatia hamasa ya kulima zaidi.
Muhono Mwikwabe mkazi wa kijiji cha Rwamchanga wilaya ya Serengeti ambaye inadaiwa alipigwa risasi na askari wa pori la akiba la Ikorongo kwa madai ya kuchungia mifugo ndani ya eneo la hifadhi hiyo na kusababisha kukatwa mguu,hapo akieleza mkasa uliomkuta na kumfanya kuwa tegemezi.
Anaendelea kueleza jinsi ambavyo alitendewa unyama huo na wahusika hawajawahi kukamatwa licha ya kufahamika |
Waandishi wa habari wakiwa wanamsikiliza Mwikwabe ambaye anategemewa na familia ya watu 20.
Kutokana na ulemavu huo hawezi kwenda shamba wala kuchunga mifugo.
Emmanuel Salinge Mwanasheria kutoka Pingo's akiwa amekaa na Mwikwabe baada ya kusikiliza mkasa uliomkuta ha kuwa polisi hawajawahi kushughulikia masuala yake ikiwemo ng'ombe wake 40 anaodai walichukuliwa na askari wa wanyama pori wa Ikorongo.
Kutokana na vyanzo vya maji kuchukuliwa na kuwa ndani ya Pori la Ikorongo wakazi wa vijiji vya Rwamchanga,Bonchugu na maeneo yaliyoko pembezoni mwa pori hilo wanalazimika kusomba maji na kuwanywesha ng'ombe kwa kuogopa kukamatwa.
Adha ya maji
Vijana kutoka kijiji cha Bonchugu wilayani Serengeti
Mnadani Mugeta wilayani Bunda biashara ya Ng'ombe ni kubwa kwa kuwa watu hutoka maeneo mbalimbali kwa ajili ya kununua ng'ombe .
Wanatolewa mnadani
Biashara inaendelea hapo wanalipana baada ya kuuziana ng'ombe
Baada ya manunuzi safari huanza kama inavyoonekana.
wafugaji wanajadiliana
wafugaji wa jamii ya Kitaturu wa kijiji cha Sarakwa kata ya Hunyari wilayani Bunda wakiwa kwenye kikao cha kujadili changamoto za ufugaji zinazowakabili ikiwa ni pamoja na kukosa malisho na maji
0 comments:
Post a Comment