Godfrey Msagati(23)mkazi wa Mugumu wilaya ya Serengeti anahitaji msaada wa pesa ili aende Oceon Road kwa matibabu ya Kansa ,hapo yuko na mama yake mzazi,picha na Serengeti Media Centre
Posted Ijumaa,Marchi27 2015
Posted Ijumaa,Marchi27 2015
Kwa ufupi
Nashon mzaliwa wa Mugumu Wilaya ya
Serengeti kwa kipindi cha miaka saba, alikuwa akifanya kazi na kampuni moja ya
Kichina iliyopo nchini.
Geofrey Msagati (23), ni Fundi
Seremala ambaye ndoto za siku moja kufungua kampuni yake zimezimika na wala
hajui hatima ya maisha yake kutokana na maradhi yanayomsibu.
Nashon mzaliwa wa Mugumu Wilaya ya
Serengeti kwa kipindi cha miaka saba, alikuwa akifanya kazi na kampuni moja ya
Kichina iliyopo nchini.
Kampuni hiyo ilishiriki kujenga
majengo mbalimbali nchini ikiwamo Hoteli ya Kiwanda cha Saruji cha Kigamboni
pamoja na hoteli kadhaa za kitalii Zanzibar na Mtwara, pia nyumba za
wafanyakazi wa mradi wa gesi Mtwara.
Kwa sasa ‘yupo gizani’ kutokana
sehemu kubwa ya maisha yake kuitumia akiwa kitandani.
Hali hiyo kwa Msagati ambaye ni
mkazi wa Mtaa wa NHC mjini Mugumu, mkoani Mara inatokana na maradhi
yanayoelezwa kuwa ni saratani iliyosababisha mguu wake kuvimba tangu unyayo
hadi pajani, hata kushindwa kutembea wala kuvaa nguo.
Anaeleza kwamba alikutwa na mkasa
huo alipokuwa kazini, wakati akiweka ‘jipsum’ katika moja ya nyumba za
wafanyakazi wa mradi wa gesi Mtwara.
“Machi mwaka jana nikiwa na wenzangu
mkoani Mtwara katika ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa mradi wa gesi, mguu
wangu uliteleza kutoka mbao nilizokuwa nimekanyaga na moja ikanigonga mguuni
eneo la ugoko… nilihisi maumivu makali, lakini baadaye nikaendelea na kazi,”
anasimulia Msagati huku akiugulia maumivu.
Anasema siku hiyo aliendelea na kazi
bila kujua kama madhara yake yatakuwa kama yalivyo sasa, lakini bahati mbaya
mwajiri wangu hakutaka nikachunguze afya yangu.
“Kumbe walinihitaji mimi kwa
utaalamu wangu, wala hawakujali afya yangu…. sasa nakufa huku nakijiona na
hakuna msaada wowote kutoka kwao,” anasema huku akitokwa na machozi.
Msagati anaeleza kuwa matibabu
aliyokuwa akipata ni dawa za maumivu, huku akiendelea na kazi na kwamba hata
alipoomba fedha kwa ajili ya matibabu hakupewa na kulazimika kujitibu na
baadaye akapewa nauli ya kumrudisha Dar es Salaam.
Anaeleza kuwa akiwa huko alipata
huduma na dawa za maumivu hali ikawa nzuri na kurejea Zanzibar kwenye ujenzi wa
hoteli moja ya kitalii.
“Nikiwa Zanzibar maumivu yalianza
tena nikaenda Hospitali ya Mnazi Mmoja, nikapigwa X-ray wakasema nyonga na
mifupa iko sawa na kwamba huenda ni mishipa haijakaa vizuri. Nikapewa dawa za
maumivu, lakini hali ikazidi kuwa mbaya ndipo nikarudishwa Dar es Salaam bila
msaada,” anasema.
Anaeleza kuwa alirudishwa Dar es
Salaam huku akitembea kwa kuchechemea kutokana na maumivu, ndipo Oktoba mwaka
2014 alipoona hali inazidi kuwa mbaya aliomba atumiwe nauli na mama yake ili
aweze kurudi nyumbani.
Msagati anasema Desemba mwaka jana
mguu wake ukaanza kuvimba huku uwezo wa kutembea ukipungua. Alikwenda Hospitali
Teule ya Nyerere, Wilaya ya Serengeti ambako madaktari walimpa rufaa kwenda
KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro kwa mabingwa wa mifupa.
“Hatukwenda kwa wakati kwa kuwa mama
alikuwa ameishiwa fedha. Ikabidi mama aanze kazi ya kuomba kwa msaada kwa watu
mbalimbali na makanisani. Tulipopata fedha Februari mwaka huu, nikapelekwa KCMC
na madaktari walisema nina saratani kwenye mifupa, hivyo nipelekwe Taasisi ya
Saratani Ocean Road Dar es Salaam,” anasema Msagati na kuongeza:
“Tatizo ni fedha maana naishi na
mama ambaye anafanya biashara ndogondogo. Kuna wadogo zangu wanasoma, naye kwa
kipindi chote hafanyi kazi maana ndiye anayenibeba kila hatua, kampuni
niliyofanya kazi haijanisadia wala haikutaka kutupatia mikataba ya kazi, hivyo
nashindwa nianzie wapi.”
Kilio cha mama
Mama wa Msagati, Lucy Magere anasema
anachokiomba kwa sasa kutoka kwa Watanzania ni kunusuru maisha ya kijana wake
kwa kuwa hana uwezo wala namna ya kufanya kutokana na umaskini huku akiishi kwa
misaada ya watu wanaofika kumjulia hali mgonjwa.
“Kwa kipindi chote niko ndani
namhudumia Msagati, sina muda wa kutoka hata kufanya ujasiriamali, mtaji
wenyewe umeisha… maana hivi nililazimika kukaa hospitali kwa muda mrefu
kutokana na hali yake kuwa mbaya,” anasema.
Anaomba wanaoguswa wamsaidie huku
akiishauri Serikali kufuatilia kampuni za kigeni kwa kuwa hazitoi mikataba kwa
wafanyakazi wake na wanapopata matatizo haziwasaidii.... “Kijana wangu kakaa na
kampuni kwa miaka saba, lakini ameugua wamemtekeleza na mimi ndiyo nahangaika.”
Msagati anasema licha ya kuugua,
mabosi wake hao huwa wamampigia simu mara kwa mara wakimtaka arudi kazini.
Kwa watakaoguswa wawasiliane kwa
simu namba 0787 337562 au 0768522546.
0 comments:
Post a Comment