Fahari ya Serengeti

Tuesday, May 5, 2015

ADHA YA BARABARA YA BUTIAMA HADI MUGUMU SERENGETI ILIYOAHIDIWA KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI TOKA MWAKA 2005.

 Daraja la Kyarano wilaya ya Butiama wakati wa mvua magari hushindwa kuvuka kama inavyoonekana hapa,eneo hilo liko kilometa chache kutoka nyumbani kwa hayati Baba wa Taifa Julius Nyerere.
 Mei Mosi baadhi ya wafanyakazi bora kutoka wilaya ya Serengeti walichelewa maadhimisho hayo yaliyofanyika kimkoa wilaya ya Butiama kutokana na maji kujaa .
 Hata waenda kwa miguu walipata shida zaidi
 Si Kyarano tu hata eneo la Issenye wilayani Serengeti hali ilikuwa mbaya kama inavyoonekana,barabara hiyo imekuwa ikitajwa kila wakati kujengwa kwa kiwango cha lami,ambapo mwaka 2005 ilikuwa katika ilani ya CCM,na mwaka 2010 lakini hakuna lami iliyokwishawekwa .
 Abiria wanatozwa nauli kubwa kwa kisingizo cha kuwa barabara ni mbovu
 Wafugaji hawa walikumbwa na adha hiyo na kulazimika kupitisha mifugo yao kwenye maji bila kujua kina chake katika eneo la Issenye.
 Zoezi la kupita lilikumbwa na sokomoko kubwa
 Kadri walivyokuwa wansonga hali ilizidi kuwa ngumu kwao.
 Baadhi ya mifugo ililazimika kuogelea ili kunusurika na kusombwa na maji.
 Baadhi ya ng'ombe walisombwa na maji na kulazimu wafugaji kujitosa kusaidia kuwanusuru
 Hapo wafugaji wanahangaika kumwokoa ng'ombe mmoja aliyekuwa amesombwa na maji
 Jitihada za kumnusuru ng'ombe huyo zilizaa matunda kama inavyoonekana
 Huzuni iliyokuwa imewakumba iligeuka furaha ,lakini tatizo ni barabara
 Mbwa naye alikuwa akishuhudia sakata hilo.
 Hatimaye anatoka
 Ng'ombe huyo katoka
Safari inaendelea baada ya kumwokoa ng'ombe wao.

0 comments:

Post a Comment