Feb.16,2015.
Serengeti:Mwanamke aliyepotea feb
9,mwaka huu katika mazingira ya kutatanisha katika kijiji cha Ikoma robanda
wilaya ya Serengeti Mkoa wa Mara amepatikana ndani ya hifadhi ya Taifa ya
Serengeti akiwa mzima.
Kupatikana kwa Nyangi
Sagoche(30)kumethibitishwa na uongozi wa kijiji,polisi na mganga mfawidhi wa
zahanati ya Robanda alikolazwa kwa matibabu,kumekuja huku wakazi wawili wa
kijiji hicho wakiwa wamelazwa hospitali Teule ya wilaya ya Nyerere baada ya
kupigwa na wananchi wakituhumiwa kujihusisha na vitendo vya ushirikina kijijini
hapo.
Akiongea na Blog hii kwa
kugugumia kutokana na kudhoofika wakati
amelazwa katika zahanati ya Robanda Nyangi alisema ,aliokotwa na dreva wa gari la Kampuni ya Thomson pembeni
mwa barabara lililokuwa na wageni ,ikiwa ni siku ya sita akizunguka ndani ya
hifadhi hiyo yenye wanyama wakali bila kujua alivyofika huko.
“Sijui nilifikaje huko,maana
nakumbuka februari 9 usiku nikitoka senta kwenda nyumbani niliitwa na mzee
mmoja anayeishi kitongoji cha Mereshi anajishughulisha na kucheza ngoma za
asili…akanilazimisha kwenda kunywa pombe,nilikataa akasema umenikatalia
haya,hapo ndipo nilipoteza fahamu na sijui ilikuwaje hadi leo(jana)nilipookotwa”alisema.
Alisema kwa siku zote sita
hakuwahi kula wala kunywa lakini akawa ni mtu wa kutembea porini huku wanyama
wakali kama Simba ,tembo ,nyati na Fisi
akipishana nao,usiku akilala kwenye
miti,”ramani ya nyumbani nikawa siijui,hata sijui nilifikaje pembeni mwa
barabara nikaa chini ya mti hadi nilipookotwa,si tukio la kawaida najua
lililonikuta”alisema bila kufafanua.
Kwa kipindi chote alikuwa
akilalamika njaa na kuwa mwili wake umejaa miiba,hata hivyo licha yakutembea
porini bila viatu , hakuwa na jeraha la kuchomwa na miiba hali iliyozidisha
maswali kutoka kwa wananchi.
Mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo
Christopher Charles alisema Nyangi alifikishwa kituoni hapo akiwa amedhoofika
sana na kuwekewa maji kwa muda mfupi chupa tatu zikawa zimeisha na kuomba
kukojoa ikiwa ni dalili kuwa alikuwa ameishiwa maji.
“Kwa kwa mwanamke akikaa siku
saba bila kula ama kunywa chochote anaweza kufa,huyu alikuwa akitumia akiba ya
chakula chake mwilini,na kilikuwa kinaelekea kuisha kabisa ,tatizo alilonalo ni
hilo tu,maana akili iko vizuri,hana jeraha sehemu yoyote katika mwili
wake”alisema.
Akizungumzia tukio hilo mme wake
Marekanyi Charles(31)alisema tukio hilo si la kawaida kwa kuwa amepatikana
ikiwa ni siku moja tu baada ya watu wanadaiwa kujihusisha na mambo ya
ushirikina kutajwa na kuadhibiwa ,wengi wakirudisha mikoba yao,miongoni mwao
akiwemo baba yake mzazi.
“Huyu mwanamke tulikuwa
tumetengana naye kwa muda,lakini akitoka hapa hospitali itabidi arudi nyumbani
tuishi na tulee watoto wetu watatu,maana nimegundua kuwa huyu mwanamke alikuwa
anazongwa na mambo yasiyo ya kawaida”alisema.
Afisa Mtendaji wa kijiji hicho
Itabe Nkiri alisema kwa muda wa siku nne shughuli mbalimbali za uchumi kwa
ajili ya msako wa huyo mwanamke ,hivyo kupatikana kwake kunaleta nafuu kijijini
na kuomba jamii iachane na imani za kishirikina bali wamrudie Mungu.
“Mambo ya ushirikina yanashika
kasi sana hapa maana februari 7 kijana mmoja Matiko Mkeya alipotea na tarehe
8 mwezi huu akapatikana akiwa amefungwa
sanda….watu waliotajwa na jamii waliadhibiwa,siku ,moja tu likatokea hili kuna
kila sababu ya jamii ikae iweze kuonyana maana madhara yake ni makubwa ,watu
kuhasimiana na kupoteza muda wa kuzalisha mali”alisema.
Mwenyekiti wa Jamii ya Waikoma kijiji
cha Robanda Masauta Shitabara alisema tukio la kupatikana kwa Nyangi akiwa hana
jeraha wala michubuko kilometa 16 ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti
linazua maswali na kudai akipatana ahueni wataitisha kikao ili awaambie
wananchi kilichotokea kwa kuwa kumeibuka matukio yasiyo ya kawaidia kijijini
hapo.
“Amepatikana siku tuliyotangaza
mapumziko ,ikiwa siku moja tu watu 19 wamebanwa na jamii kutokana na
kujihusisha na vitendo vya kishirikina,wapo waliorudisha mikoba yao ikiwemo
mafuta ya mtu,ngozi ya mtoto,na dawa mbalimbali,na baada ya kupatikana kwa huyu
katika kikao cha jamii tutaelezana mambo mengi”alisema.
Kwa upande wake Paroko wa Parokia
ndogo ya Fort Medard Chegere akimwombea Nyangi hapo Zahanati aliwataka wamrudie
Mungu wa kweli waache kuabudu Miungu kwa kuwa hayo ndiyo matokeo yake,matukio
hayo yawe fundisho kwao.
Wakati huo huo katika kijiji cha
Miseke kata ya Manchira wilayani hapa alipatikana mwanamke mmoja akiwa hawezi
kuzungumza kwa madai kuwa amekatwa ulimi ,huku wengine wakidai ni msukule ikiwa
haijulikani alikotokea.
Mchungaji wa kanisa la Anglikana
Miseke Sedekia Chikumbiro na Mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo Mturi Mtumbe
walisema baada ya kumchunguza walikuta ulimi umekatwa na ndiyo maana hawezi
kuongea,kwa kuwa akili yake iko vizuri kwa kuwa akiona watu anaona aibu lakini
hawezi kuzungumza kwa ufasaha.
Kamanda wa polisi wilaya ya
Serengeti Pius Mboko aliwataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi
,badala yake matukio yote yashughulikiwe kwa misingi ya kuheshimu misingi ya
Haki za Binadamu.
Mwisho.
NYANGI MKAZIWA KIJIJI CHA ROBANDA WILAYA YA SERENGETI ALIYEPOTEA JANUARI 9 USIKU AKITOKA KWENYE KILABU CHA POMBE ,HATA VIVYO MSAKO WA JAMII ULIAMBULIA MALAPA,CHUPI .JUHUDI ZA KUMSAKA KIJIJINI NA PORINI KWA MUDA WA SIKU TANO HAZIKUZAA MATUNDA HADI FEB 15 MAJIRA YA ASUBUHI ALIPOKUTWA NA GARI LILILOKUWA LIMEBEBA WAGENI NDANI YA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI AMEKAA,HAPO YUKO KITUO CHA AFYA ROBANDA AKIPATA HUDUMA ,KWA MJIBU WA MGANGA MFAWIDHI CHRISTOPHER CHARLES AMESEMA MWANAMKE HUYO HANA JERAHA LOLOTE BALI ALIKUWA NA TATIZO LA KUISHIWA NGUVU KUTOKANA NA KUTOKULA KWA MUDA MREFU.
ANAPATA HUDUMA
NDUGU ZAKE NA WAKE ZA SHEMEJI ZAKE WAKIMHUDUMIA
MGANGA MFAWIDHI WA KITUO AKIMHUDUMIA
ANASINDIKIZWA KWENDA KUJISAIDIA
ANANYWESHWA UJI
PADRI MEDARD CHEGERE PAROKO WA PAROKIA NDOGO YA FORT AKIMWOMBEA
MAOMBI YANAENDE;EA
0 comments:
Post a Comment