Fahari ya Serengeti

Wednesday, August 6, 2014

TEMBO WAONGEZEKA MAPORI YA AKIBA YA IKORONGO/GURUMETI



Tembo
Agosti,2014
Wakati Tembo katika mapori mengi ya akiba wakidaiwa kupungua,hali ni tofauti kwa Mapori ya akiba ya Ikorongo na Gurumeti wilayani Serengeti wameongezeka kutoka 355 hadi 1,236 kwa kipindi cha mwaka miaka kumi.
Ongezeko hilo ni sawa na tembo 84 kwa kila mwaka linachangiwa na ulinzi madhubuti wa askari wa mapori hayo kwa kushirikiana na Kampuni ya Gurumeti Reserves ambao wamekodi vitalu hivyo.
Mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mahamod Mugimwa hivi karibuni  ,Meneja wa Mapori hayo Nollasco Ngowe akitoa taarifa kuhusu mapori hayo alisema ,walifanya sensa mwaka 2003 wakapata tembo 355 na mwaka 2013 ikiwa ni baada ya miaka kumi wamepata tembo 1,236,ikiwa tofauti na mapori mengine  ambayo idadi hushuka.
“Pamoja na changamoto tulizonazo za upungufu wa askari ,magari na wingi wa vituo…migogoro ya tembo na wakulima….bado ulinzi umekuwa madhubuti hali ambayo inasaidia kudhibiti majangili”alisema.
Meneja huyo alisema ili kuimarisha ulinzi katika mapori hayo aliomba wizara kuwaongezea askari na magari,kwa kuwa askari waliopo ni wachache  kulingana na kazi za ulinzi,kufukuza tembo,doria na kuongoza watalii wa kupiga picha katika mapori hayo.
Kuhusu uharibifu wa mazao alisema hilo ni tatizo kubwa kwa vijiji vinavyowazunguka ,”kwa kushirikiana na Kampuni ya Gurumeti Fund kama serikali itatoa kibali wako tayari kutumia risasi za pilipili zinazopigwa usoni….inapomuwasha tembo anakimbia na hataweza kurudi eneo hilo…pia kutumia bunduki aina shortgun….kuna tafiti zimeonyesha njia hiyo imesaidia”alisema.
Alibainisha kuwa  baadhi ya tembo wamekimbia Masai Mara na kuingia Tanzania ambao huenda wanachangia kuingia kwenye mashamba kwa wingi,”hilo tunalitafiti,lakini  pia  wananchi kutokufuata sheria inayowataka walime mita 500 kutoka mpaka wa hifadhi,”alisisitiza.
Kuhusu mapato yaliyokusanywa kutokana na utalii wa kupiga picha alisema wageni 4020 waliingia na kufanikiwa kukusanya dola za Kimarekani 1,195,540 kwa kipindi cha mwaka wa fedha wa 2013-14.
Akizungumzia maombi hayo  Naibu waziri Mgimwa alisema   kwa kuwa wanatarajia Mamlaka ya Wanyama Pori kuanza wakati wowote  wizara imefanya  usaili kwa askari 495,hivyo wapo watakaopelekwa kwenye mapori hayo kuimarisha ulinzi.
Kwa suala la udhibiti wa tembo wanaovamia mashamba,aliwataka waachane na njia zingine za risasi za pilipili kwa kuwa haina faida kwa jamii,bali watumie njia ya nyuki yenye faida kwa jamii”imebainika nyuki ni njia nzuri ya kudhibiti tembo….wananchi wanapata asali…huku wakidhibiti tembo,hiyo ni faida”alibainisha.
Alisema wizara iko tayari kusaidia wananchi kwa kutumia mizinga ya udongo ambayo inalenga kuhifadhi zaidi mazingira,na kumtaka Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kuhakikisha vikundi ama mashirika yasiyo ya kiserikali yanahusika ili mtandao wa mizinga uzibe kote.
Hata hivyo alitaka waangalie kati ya mabilioni yanayokusanywa kiasi gani kinarudi kwa wananchi ili waone faida za uhifadhi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Goody Pamba alisema kwa kushirikiana na shirika la Sederec ,Gurumeti Fund wameanza kutumia njia hiyo kwa baadhi ya vi

0 comments:

Post a Comment